Thursday, 1 December 2016

Sheria ya kukata 15% za mkopo wa HESLB yasainiwa


Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli tayari amekwishasaini mabadiliko ya sheria yanayomtaka mwajiri kukata asilimia 15 ya mshahara wa mwajiriwa ambaye ni mnufaika wa mkopo wa elimu ya juu kwa ajili ya kulipa deni lake analodaiwa na Bodi ya Mikopo
Mhandisi Stella Manyanya akiwa
Kikaangoni
Taarifa hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mhandisi Stella Manyanya, ambapo amesema kuwa makato kkiwango hicho kimepanda kutoka asilimia 8 ya sasa.
Akijibu maswali ya wananchi kupitia kipindi cha KIKAANGONI kinachoendeshwa kupitia mtandao facebook wa East Africa Television, Naibu Waziri Manyanya amesema sheria hiyo tayari imesiniwa na siku za hivi karibuni itaanza kutumika.
"Hii asilimia 15, kimsingi sheria ninavyofahamu ilishasainiwa, baada ya hapo kuna kuiangalia iendane na kanuni zetu, baada ya kuicheki imeendana na kanuni zetu kama kuna sehemu itahitaji kuboreshwa kidogo haitazidi miezi miwili au mitatu, baada ya hapo tutaweza kutumia hiyo 15%, na asilimia 15 ya safari hii ni tofauti na siku za nyuma, siku za nyuma tulikuwa tunachaji asilimia 8”, amesema Manyanya.
Hapo awali wadaiwa hao wa mikopo walikuwa wanakatwa asilimia 8, lakini sheria ya sasa itaruhusu wadaiwa wa mikopo ya elimu ya juu kukatwa asilimia 15 ya kipato chao.
Pia Manyanya amesisitiza kuwa kwa wale ambao hawajaajiriiwa, lakini wanafanya biashara zao wanatakiwa kuwasilisha angalau shilingi 120,000 kila mwezi na kuwashauri kuwa ni vema wakapeleka zaidi ili wamalize haraka madeni yao.
Kuhusu wasio na kazi, amesema haiwezekani mtu asome halafu akose shughuli ya kufanya na kuwataka kutafuta shughuli yoyote ya kufanya ili waanze mapema kulipa madeni yao ndani ya miaka miwili baada ya kuhitimu  masomo.
Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *