Thursday, 1 December 2016

FA YAMTANGAZA GARETH SOUTHGATE KUWA KOCHA MKUU WA ENGLAND


gareth-southgate-england-u21s-under-21s-u21-press-conference_3373168

Gareth Southgate amechaguliwa rasmi kuwa kocha mkuu  wa  timu ya Taifa ya England kwa kumpa mkataba wa mika minne aliosaini.
Southgate mwenye umri wa miaka 46 aliacha wadhfa wake kama mkufunzi wa timu ya England ya vijana wasiozidi miaka 21 mnamo mwezi Septemba baada ya aliyekuwa meneja wa Uingereza Sam Allardyce kujiuzulu baada ya kuhudumu kwa siku 67 pekee.
Aliisaidia Uingereza kushinda mara mbili pamoja na sare mbili kama kaimu mkufunzi na sasa ametia saini kandarasi ya miaka minne yenye thamani ya pauni milioni 2 kwa mwaka.
”Nimefurahia sana kushirikiana na wachezaji katika mechi nne na ndhani kuna vipaji vingi”,alisema.
Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *