Marekani yapendekeza vikwazo dhidi ya viongozi wa Sudan Kusini | MASWAYETU BLOG
Breaking News
Loading...
Millionaire  Ads

Sunday, 20 November 2016

Marekani yapendekeza vikwazo dhidi ya viongozi wa Sudan Kusini


media
Mjumbe wa Marekani kwenye baraza la usalama la umoja wa Mataifa Samantha Power.
Marekani imependekeza azimio kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kutaka Sudan Kusini kuwekewa vikwazo vya kununua na kuingiza silaha.
Aidha, azimio hilo linapendekeza watu binafsi kutoka upande wa serikali inayoongozwa na rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar kuwekewa vikwazo.
Marekani inasema kwamba kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini Riek Machar, mkuu wake wa majeshi na waziri wa habari wawekewe vikwazo na Umoja wa Mataifa kwa kuchochea vita nchini humo.
Kwa mujibu wa ujumbe uliopatikana na AFP Machar, mkuu wa majeshi ya rais Salva Kiir, Paul Malong na waziri wake wa habari Michael Makuei wako kwenye orodha nyeusi ya vikwazo.
Chini ya hatua iliyopendekezwa, Macha ambaye anapatiwa matibabu nchini Afrika Kusini na maafisa hao wawili watakabiliwa na vikwazo vya kusafiri na mali zao kuzuiwa.
Hatua hii imekuja baada ya watalaam na Umoja wa Mataifa kuonya kuwa huenda kukatokea kwa mapigano na mauaji ya halaiki nchini humo katika siku zijazo ikiwa hatua haitachukuliwa.
Azimio hilo sasa linasubiri kura kutoka kwa wanachama wa Baraza hilo, licha ya kuwepo kwa wasiwasi huenda Urusi ikatumia kura yake ya Veti na kuzuia kupitishwa kwa azimio hilo
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APPLICATION MPYA YA MASWAYETU BLOG

google+

linkedin

About Author
  • Donec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Sed posuere consecteturDonec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Read More

    0 comments:

     

    About Us