Saturday, 12 November 2016

HIZI HAPA KURASA ZA NDANI MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI NOV 12 20161
2
3
4
5
6
7
8
9

1
2
3
4
5
6
7
8
9
10

Magazeti ya Leo Jumamosi

Published in Jamii

AZAM FC KUSUKA KIKOSI CHA NGUVU RAUNDI YA PILI

Published in Jamii
rodrogo
Kocha Mkuu, Zeben Hernandez kulia na Kocha Msaidizi wa Azam FC, Yeray Romero.
............................................................
UONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, kwa kushirikiana na benchi la ufundi la timu hiyo hivi sasa upo kwenye mchakato wa kukiongezea nguvu kikosi hicho.
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni nia ya dhati kabisa ya Azam FC kutaka kufanya vizuri zaidi kwenye mzunguko wa pili wa ligi, Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) na michuano ya Kimataifa inayokuja kuanzia mwezi ujao na mwakani (Kombe la Kagame na lile la Shirikisho Afrika).
Mabingwa hao wa Ngao ya Jamii mwaka huu, tayari wamemaliza mzunguko wa kwanza wa ligi wakiwa kwenye nafasi ya tatu kwenye msimamo wakijikusanyia jumla ya pointi 25, wakizidiwa pointi 10 na kinara Simba aliyejizolea 35.
Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz juzi Kocha Msaidizi wa Azam FC, Yeray Romero, alisema kuwa kuelekea mzunguko wa pili wa ligi wanatarajia kuangalia mapungufu ya kikosi hicho kabla ya kuingiza sura mpya kwenye usajili ya dirisha dogo kwa ajili ya kuinyanyua timu na kufika kwenye nafasi nzuri zaidi.
“Wakati wachezaji wapya wanaingia pia tunatarajia kuwaangalia wachezaji ambao tunadhani kwa sasa kikosini hawawezi kuisaidia timu, ambao ndio watawapisha wachezaji hao, lengo la yote haya ni kuweza kuipeleka mbele zaidi timu zaidi ya hapa ilipo,” alisema.
Katika hatua nyingine, Romero aliwapongeza wachezaji kwa kazi waliyoweza kuifanya mpaka sasa huku wao kama benchi la ufundi wakiahidi kufanya kazi nzuri zaidi kwa asilimia 100 katika kuirekebisha zaidi timu na kuziba mapungufu yaliyopo.
Matarajio yamefikiwa?
“Kiufupi matarajio hayakuwepo ya kumaliza nafasi ya tatu kwenye mzunguko wa kwanza, hatukuwa tumepanga kufika nafasi hiyo lakini mazingira tuliyokuwa nayo yametufanya kumaliza hapo, licha ya yote hii ni nafasi nzuri kwetu na tunachoangalia kwenye raundi ijayo ni kufika nafasi pili na ya kwanza,” alisema.
Kauli kwa mashabiki Azam FC
Kocha huyo wa zamani wa timu za CF Reale Juventud Laguna na CD Tenerife zote za Hispania, aliwashukuru mashabiki wa Azam FC kwa sapoti kubwa wanayoendelea kutoa kwenye mechi zao licha ya kupitia wakati mgumu kwenye baadhi ya mechi.
“Kwa kweli nachukua fursa hii kuwapongeza mashabiki wa Azam FC, kwa yote yaliyotokea wao wamekuwa pamoja nasi, timu inapofanya vibaya wapo na inapofanya vizuri wapo na ambacho tunaweza kuwaahidi ni mashabiki wetu ni kwamba waendelee kuwa na imani na timu yao kwa sababu nafasi tuliyofikia hivi sasa si mbaya sana, lakini ingawaje si kama ndio tuliyokuwa tumepanga kufika.
“Hivyo tunategemea raundi ya pili itakapoanza kwa nguvu ambazo tutaziingiza kikosini basi wakiwa wanaendelea kutusapoti kama mwanzo naamini ya kuwa mashabiki watajikuta kwamba hawakukosea kuichagua Azam FC kwa sababu matokeo yatakuwa ni mazuri kwa timu kuweza kupata ushindi,” alimalizia mtaalamu huyo.
Azam FC kuendelea kujifua
Wakati huo huo, mara baada ya kikosi cha Azam FC kurejea jana jioni jijini Dar es Salaam kikitokea mkoani Shinyanga kilipocheza na Mwadui, taarifa ni kuwa wachezaji wa timu hiyo wataendelea na mazoezi kama kawaida jioni ya leo.
Kwa mujibu wa programu ya benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Zeben Hernandez, mara baada ya mazoezi ya leo, kikosi hicho kinatarajia kucheza mchezo wa kirafiki kesho Jumamosi kabla ya kupumzika Jumapili na Jumatatu kitacheza mchezo mwingine wa kujipima ubavu.
Tathimini ya mzunguko wa kwanza
Azam FC inayodhaminiwa na kinywaji safi ya Azam Cola kinachochangamsha mwili na kuburudisha koo na Benki bora nchini kwa usalama wa fedha zako ya NMB, imefanikiwa kucheza jumla ya mechi 15 kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi ikifanikiwa kushinda jumla ya mechi saba, sare nne na kupoteza nne ikiwa imekunja kibindoni pointi 25.
Takwimu pia zinaonyesha kuwa, Azam FC imeshinda robo tatu ya mechi zake ilizocheza ugenini, ikiibuka na ushindi mara tano kati ya mechi nane za ugenini, ikifungwa tatu, kati ya mechi saba ilizokuwa mwenyeji imefanikiwa kuibuka kidedea mara mbili, sare nne na kuteleza mechi moja.
Hivyo takwimu hizo zinaeleza kuwa Azam FC imefanikiwa kupata alama 15 kwenye viwanja vya ugenini kati ya 24 ilizotakiwa kuvuna, ambapo imepoteza jumla ya pointi tisa ugenini.
Mabingwa hao wamevuna jumla ya pointi 10 kati ya 21 katika uwanja wa nyumbani, ikiwa imeacha uwanjani jumla ya pointi 11, nane katika uwanja wake wa Azam Complex kutokana na sare nne ilizotoa ndani ya dimba hilo na tatu ikiziacha ndani ya Uwanja wa Uhuru kufuatia kupoteza bao 1-0 dhidi ya Simba ambayo inaongoza ligi ikiwa na pointi 35 pungufu ya pointi 10 na mabingwa hao.
Rekodi ya ufungaji wa mabao zinaonyesha kuwa mpaka sasa kikosi hicho kimefunga 21, ukiwa ni wastani wa bao 1.4 kwenye kila mchezo katika mechi 15 ilizocheza huku pia ikiruhusu nyavu zake kutikiswa mara 14 (yaani wastani wa kufungwa bao 1.0 kwenye kila mchezo iliocheza).
Nahodha John Bocco ‘Adebayor’, ndiye ameonekana kinara wa kutupia mabao msimu huu ndani ya Azam FC mpaka sasa akitupia sita akizidiwa mabao matatu na Shiza Kichuya wa Simba aliyekuwa kileleni kwa mabao tisa, wengine wanaomzidi ni Rashid Mandawa (Mtibwa Sugar), Simon Msuva, Amissi Tambwe (Yanga), ambao wote wamefunga saba kila mmoja.
Bocco pia yupo kileleni kwenye utengenezaji wa mabao akiwa ametoa pasi za mwisho nne, akifuatiwa kwa ukaribu na Khamis Mcha aliyechangia matatu ambaye pia ametupia wavuni matatu, huku Shaaban Idd aliyeweka kambani matatu naye akipika mawili.
Mpaka raundi ya kwanza inamalizika mchezaji wa Azam FC aliyecheza mechi nyingi kuliko mwingine yoyote ni kipa namba moja, aliyecheza 14 sawa na dakika 1,260 kati ya 1,350, alizotakiwa kucheza hadi ligi inafikia katikati na hii ni baada ya kupumzishwa mechi moja wakati kikosi hicho kikikabiliana Mbao, mchezo ulioisha kwa Azam FC kuteleza kwa kufungwa mabao 2-1. (P.T)
watun
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani ambae pia ni katibu wa kamati ya usalama barabarani mkoani Pwani,Abdi Issango,(aliyeshikiwa mic)akionekana anazungumza jambo. (Picha na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
WATUNGA sera kupitia serikalini wameombwa kuangalia uwezekano wa kuzifanyia marekebisho baadhi ya sheria za usalama barabarani ikiwemo adhabu za faini zinazotolewa ziweze kuwa na maumivu kwa wakiukwaji.
Watunga sera hao wanatakiwa kuzipitia upya sheria hizo (The road traffic act cap 168) ya mwaka 1973 kwani kifungu cha 50 kulipita gari vibaya adhabu yake ni sh 1,000 na isizidi 2,000 na kifungu cha 45 dereva aliyekutwa amelewa ni sh.10,000 hadi 20,000.
Kamanda wa usalama barabarani mkoani Pwani, Abdi Issango ,aliyasema hayo wakati akizungumza na wadau wa usalama barabarani na waandishi wa habari.
Alisema baadhi ya sheria ni za zamani hivyo zinapaswa kwenda na wakati na haina budi ziangaliwe upya kwa kubadilishwa ili kwenda na hali ilivyo sasa.
Kamanda Issango alieleza kwamba sheria hizo husababisha baadhi ya watumiaji barabara hususan madereva kutokuwa na hofu ya kukiuka sheria kutokana na faini kuwa ndogo.
“Mfano wa sheria ya usalama barabarani (The Road Traffic Act Cap 168) ya mwaka 1973 adhabu nyingi ni ndogo na hazileti majuto wala hofu kwa mkosaji , ni kinyume na malengo ya adhabu ya kumpa maumivu mhusika”
“Kifungu cha 50 cha kulipita gari jingine vibaya adhabu yake ni sh. 1,000 na isizidi sh.2,000 na kifungu cha 45 dereva akitiwa hatiani kwa kosa la ulevi adhabu yake ni sh.10,000 na isizidi 20,000,” alisema Issango.
Alifafanua adhabu inatakiwa mkosaji apate majuto,hofu na maumivu ili ajutie kosa na kuogopa kosa alilotenda, hivyo kutokana na adhabu hizo kuna haja ya kuzipitia upya sheria hizo ili zitoe adhabu kali.
Issango ambae pia ni katibu wa kamati ya usalama barabarani mkoani hapo alitoa rai kwa jamii na wadau mbalimbali kuipigia kelele serikali ili iweze kubadilisha baadhi ya vifungu vinavyotoa adhabu ndogo kwa wakosaji .
Alieleza endapo adhabu zitakuwa kubwa itasababisha kuogopa ama kusita kurudia makosa kwa makusudi kwani wengine wanarudia kwa kujua adhabu siyo kali.
Issango alisema katika kukabiliana na ajali mahakama zinapaswa kutenda haki na kumaliza kwa wakati kesi zinazotokana na usalama barabarani .
Alisema pia wadau wote wanapaswa kushirikiana ili kupunguza ajali ambazo nyingine zimekuwa zikisababishwa kutokana na uzembe.
“Nawasihi madereva wa vyombo vyote vya moto kuacha kufanya mbwembwe wakiwa barabarani ,kutotumia vilevi wakati wakiendesha ,kuacha kupita magari mengine(overtake)ovyo na mwendo kasi ili kuepukana na ajali”anasisitiza . (P.T)

VETA kuanzisha kozi ya Utalii wa Kitamaduni

Published in Jamii
vet1
.Mwalimu wa Ufundi Mitambo wa Chuo cha VETA Mikumi, Peris Shao, akizungumza na waandishi wa habari juu maendeleo ya chuo hicho katika utoaji wa mafunzo ya ufundi Stadi.
vet2
Wanafunzi wakiwa katika karakana ya ufundi Mitambo wakiwa katika mafunzo ya vitendo katika Chuo cha Mikumi
vet3
Mwalimu wa uChuo cha VETA Mikumii, James Maungu akitoa maelezo kwa waandishi wa habari walipotembelea karakana ya ufundi huo.
vet4
Mwanafunzi wa mwaka wa mwisho wa Chuo cha VETA Mikumi wakiwa katika mafunnzo ya vitendo karakana ya ufundi wa Magari.
Mamlaka ya Elimu na mafunzo ya Ufundi stadi (VETA) kupitia chuo cha VETA Mikumi inatarajia kuanzisha kozi ya utalii wa kitamaduni  ili kuwafundisha watanzania  tamaduni ,mila na desturi ili kuulinda utamaduni wetu , ambao unaonekana kupotea kadri teknolojia inavyozidi kukua kila siku.
Akizungumza na waandishi wa habari walipotemebelea chuo hicho Cha VETA Mikumi, Mkuu wa chuo hicho Christopher Ayo amesema kuwa uamuzi huo umetokana     na sekta ya utalii kuendelea kukua mwaka hadi mwaka huku jamii ikionekana kusahahu uhasilia wa tamaduni mbalimbali za kitanzania .
Amesema utamaduni ukitumika ipasavyo unaweza kuchangia ukuaji wa sekta ya utalii pamoja na uchumi nchini kutokana na ukweli kwamba nchi nyingi duniani zimeweza kulinda utamaduni kuweza kukuza uchumi wao.
Amesema chuo chake kwa kushirikiana na Chuo cha NOVA Scotia Communinity College cha nchini Canada kinaanda kozi  hiyo itakayowezesha watanzania kujifunza kwa undani kuhusu utamaduni wao kama vile ngoma, vyakula vya asili ,sanaaa na historia ya makabila mbalimbali.
Ayo amesema maandalizi ya kuanzisha kozi hiyo yapo kwenye hatua za mwisho na kwamba kuanzia Januari, 2017 masomo yataanza kutolewa.
Aidha mkuu huyo amesema walimu watano watakaofundisha masomo hayo wameshaandaliwa na kupatiwa mafunzo nchini Canada jinsi ya kutumia technologia katika kufundisha na kuandaa mitaala.
Ayo amesema VETA Mikumi itaendelea kutoa mafunzo kwa jamii inayowazunguka katika kuwaandaa vijana katika soko la ajira kwa kujiajiri au kuajiriwa na kuweza kuendesha maisha yao na kuchangia pato la taifa.
Ametoa rai kwa vijana wa mikumi na maeneo ya mengine ya Mkoa wa Morogoro kuchangamkia fursa za mafunzo zilizopo chuoni hapo ili kuweza kuwa sehemu ya wataalam watakaohudumia viwanda vitakavyojengwa kutokana na serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kuweka msisitizo wa kuhakikisha nchi inakuwa ya  viwanda. (P.T)
wai1
ALIYEKUWA MKUU WA MAJESHI JENERALI MSTAAFU GEORGE WAITARA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI (Hawapo Pichani ) KATIKA KLABU YA GOLF YA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA YA LUGALO JIJINI DAR  ES SALAAM  KUHUSU MAANDALIZI YA KOMBE LA WAITARA LINALOTARAJIWA KUGOMBANIWA JUMAMOSI NOMVEMBA 19 (Picha na Luteni Selemani Semunyu)
wai2
BAADHI YA WANAFUNZI WALIOJITOKEZA KUPATA MAFUNZO YA MCHEZO WA GOLF KATIKA KLABU YA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA YA LUGALO JIJINI DAR  ES SALAAM   WA KWANZA ALIYEPIGA MPIRA NI LUTENI FADHILA NAYOPA (Picha na Luteni Selemani Semunyu)
wai3
ALIYEKUWA MKUU WA MAJESHI JENERALI MSTAAFU GEORGE WAITARA AKIZUNGUMZA NA BAADHI YA WANAFUNZI WALIOJITOKEZA KUPATA MAFUNZO YA MCHEZO WA GOLF KATIKA KLABU YA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA YA LUGALO JIJINI DAR  ES SALAAM.(Picha na Luteni Selemani Semunyu)
wai4
MCHEZA GOLF  NICHOLOUS CHINDA AKIMFUNDISHA NAMNA YA UKAAJI MMOJA WA WANAJESHI WALIOJITOKEZA KUJIFUNZA  MCHEZO HUO  KATIKA KLABU YA GOLF YA LUGALO JIJINI DAR ES SALAAM (PICHA NA LUTENI SELEMANI SEMUNYU)
wai5
BAADHI YA WANAFUNZI WALIOJITOKEZA KUPATA MAFUNZO YA MCHEZO WA GOLF KATIKA KLABU YA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA YA LUGALO JIJINI DAR  ES SALAAM   WAKIANGALIA  NAMNA YA UPIGAJI MPIRA (PICHA NA LUTENI SELEMANI SEMUNYU).
Na Luteni  Selemani Semunyu JWTZ

Aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Mstaafu George Waitara amesema wakati umefika sasa kwa Michezo ya  Majeshi kwa nchi za Afrika Mashariki kujumuisha mchezo wa Golf kutokana na idadi kubwa ya maofisa na Askari wanaojitokeza kucheza mchezo huo katika Nchi hizo.
Aliyasema hayo Leo  Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari kufuatia kuanza kwa Maandalizi ya Kombe la Waitara linalotarajiwa kufanyika Novemba 19 Mwaka huu katika Viwanja vya Jeshi vya Lugalo.
“Ukiangalia Uongozi mpya na mkakati iliofanya na idadi kubwa ya Maofisa na Askari walioanza kujitokeza kujifunza mchezo huo ni ishara tosha kuwa wakati umefika kwa mchezo huo kuingizwa katika michezo itakayoshindaniwa katika Michezo ya majeshi kwa kuwa na nchi nyingine pia wapo,Alisema Jenerali Waitara.
Aliongeza kuwa ni furaha yake ikiwa ni miaka kumi tangu kuanzishwa na mwitikio kuwa mkubwa hivyo anaimani miaka ijayo kutakuwa na idadi kubwa zaidi na hivyo kuomba waaandishi wa habari kuendelea kuutangaza mchezo huo.
Akizungumzia Maandalizi ya Mashindano ya Kombe lake aliahidi kikundi chake kinachocheza ndani ya Klabu ya Lugalo na “Generals Four Balls” kitafanya vizuri katika mashindano hayo licha ya umri mkubwa walionao.
Aliwataja washiriki wa Kikundi hicho kuwa ni Yeye Binafsi Jenerali Mstaafu Waitara, Balozi Charles Sanga , Dk Edmund Mndolwa na Katibu Mkuu wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh Job Masima na kuwataka wengine pia kuanzisha vikundi vya Ushindani ndani ya Klabu ili kuongeza hamasa.
Jenerali Waitara aliwataka wachezaji wengi kujitokeza kushiriki katika  mashindano hayo kutokana na historia yake lakini kupunguza gharama kwa wachezaji kwa kuwa uwanja pekee wa kizalendo nchini huku gharama zikiwa chini  ukilinganisha na viwanja vingine.
Kwa Upande Wake Balozi Charles Sanga alishukuru  JWTZ kwa kuamua kuanzisha uwanja lakini pia kwa mwanzilishi wa Uwanja kutokana na Ukweli kuwa Uwanja Wa Golf wa Lugalo umekuwa kimbilio kwa Watu wote kutokana na uzuri wake na gharama kuwa za chini. (P.T)
Hivi ndivyo moto mkubwa ulivyokuwa ukiwaka katika Bohari la 7 General Enterprises ambapo walikuwa wakihifadhia Mataili, mchana eneo la Mikocheni Jijini Dar es salaam.

Vikosi mbalimbali vya zima moto kutoka Serikali na Makampuni binafsi wakiendelea na juhudi za kuuzima moto huo.

 Baadhi ya watu mbalimbali wakiendelea kushuhudia tukio hilo la kuteketea kwa Bohari

 Moto Mkubwa ukiendelea kuwaka

Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Suzan Kaganda akizungumzia kwa ufupi tukio hili na kusema kuwa kwa sasa hawezi zungumza chochote mpaka moto utakapozimwa kabisa 

Hapa mpaka Trekta nalo lilihusika katika kuhakikisha moto huo unazimika

 Mmoja wa waandishi wa Habari ambaye hakujulikana anatokea katika chombo gani akiwa anaendelea kutafuta sehemu nzuri ya kuchukua taarifa. (P.T)
Read more...

MDAHALO UINGEREZA KUHUSU ARDHI

Published in Jamii
UK Tanzania Diaspora summit UK 2016
TANGAZO LA MDAHALO KUHUSU ARDHI TANZANIA
Wana Diaspora wa UK manalikwa kuhudhuaria kongamano litakalojadili mstakabali mzima wa haki ya Mwana Diaspora kikatiba ikiwemo haki ya kumiliki ardhi Tanzania iwapo wewe ni mzawa.
Mdahalo unatarajia kutoa elimu na mapendekezo juu ya swala hili. Patakuwepo na wataalam mbalimbali wa maswala haya.
Karibu University of Coventry, School of Engineering
TAREH 3 December 2016
Saa 4 asubuhi
Uwepo wenu ni mhimu. Umoja ni nguvu
Kwa tarifa zaidi walisiliana na simu +44 7960811614
Ahsanteni
WOTE MNAKARIBISHWA  (P.T)

VIDEO: UTARATIBU WA KUMUAGA SPIKA SITTA BUNGENI

Published in Jamii
mwanz
Na Daudi Manongi, MAELEZO
Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) imekusanya shilingi bilioni 8.1 katika robo ya kwanza ya mwaka 2016 ikiwa ni zaidi ya shilingi bilioni 1.6 ya robo ya kwanza ya mwaka 2015 ambapo ilipata mapato ya zaidi ya shilingi bilioni 6.5.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Bw.Masanja Kungu Kadogosa wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Bwana Masanja anasema kuwa huduma ya usafirishaji abiria imezalisha mapato ya wastani wa shilingi bilioni 1.1 katika kipindi cha mwaka 2016 na Wastani wa shehena kwa robo mwaka imeongezeka na kufikia tani 63,251 ukilinganishwa na tani 48,681 zilizosafirishwa katika kipindi kama hicho mwaka jana.
Aidha kati ya mwezi Juni hadi Octoba mwaka 2016 kampuni imetekeleza miradi midogo kadhaa ya kujenga michepuo ya reli kwenda kwenye viwanda vya wateja wa TRL wenye kuzalisha shehena,ambapo Baadhi ya miradi ya reli za michepuo zilizojengwa ni kwenda kiwanda cha mbolea cha Yara kilichopo Kurasini na kiluwa Group ya Mlandizi huku michepuo mingine inatarajiwa kujengwa kuelekea viwanda vya Saruji vya Rhino na Sungura vilivyopo mkoani Tanga.
Aidha Bw.Kadogosa amesema kuwa wamefanikiwa kufanya ukarabati wa mabehewa ya mizigo 120 yaliyogharimu shilingi milioni 700 na kusema kama yangefanyiwa ukarabati nje ya nchi yangegharimu shilingi bilioni 26.
Mbali na hayo menejimenti ya TRL inaendelea kutoa kipaumbele katika kutatua madai ya wafanyakazi wake ikiwemo kuwasilisha Michango katika mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF),WADU na Saccos NMB ambapo baada ya kuwasilisha makato wafanyakazi wameanza kupata huduma stahiki.
Aidha malimbikizo ya nyongeza ya mshahara yameshatengewa shilingi milioni 600 ambazo zimelipwa ikiwa ni awamu ya tatu na menejimenti inajipanga kumaliza awamu nyingine zilizosalia.
Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa wadau na wananchi kuhakikisha wanalinda miundombinu ya reli na kuripoti mara moja kwenye vyombo vya dola wale wote wanaohujumu miundombinu kwa manufaa binafsi.(P.T)
jiatu
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Ashatu Kijaji akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika mkutano wa tano wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma.
Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imesitisha kuweka dhahabu kama hazina ya rasilimali za kigeni kwa sababu ya kuyumba kwa bei ya madini hayo katika soko la dunia na kusababisha uwezekano wa kupunguza thamani ya hazina ya rasilimali ya nchi.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Ashatu Kijaji alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Igunga Mhe. Dalaly Kafumu aliyehitaji kufahamu sababu za Serikali kukataa kutunza dhahabu safi katika Benki Kuu wakati Tanzania ni nchi mojawapo inayozalisha dhahabu safi.
Mhe. Kijaji amesema kuwa jukumu la msingi la Benki Kuu ni kuandaa na kutekeleza Sera ya Fedha inayolenga kuwa na utulivu wa bei kwa ajili ya ukuaji endelevu wa uchumi wa Taifa hivyo ili kufanikisha azma hiyo Benki Kuu inadhibiti ongezeko la ujazi wa fedha kwa kutumia nyenzo mbalimbali zikiwemo za kuuza dhamana na hati fungani za Serikali pamoja na kushiriki katika soko la jumla la fedha za kigeni kati ya mabenki.
“Katika kutekeleza jukumu lake la msingi, Benki Kuu hutunza hazina ya rasilimali za kigeni zinazotosha kuagiza bidhaa nje kwa kipindi kisichopungua miezi minne lakini kwa muda mrefu sasa Benki Kuu ya Tanzania haiweki dhahabu kama sehemu ya rasilimali hizo kutokana na kuyumba kwa bei ya dhahabu katika soko la dunia”, alisema Mhe. Kijaji.
Naibu Waziri huyo ametoa mfano wa kushuka kwa bei ya dhahabu katika soko la Dunia ambapo dhahabu ilishuka kutoka dola 1,745 za kimarekani katika mwezi Septemba 2012 hadi dola za kimarekani 1,068 kufikia mwezi Desemba 2015.
Mhe. Kijaji amefafanua kuwa hazina ya rasilimali za kigeni zinaweza kuwa dhahabu – fedha (monetary gold) au fedha za kigeni ambapo uamuzi kuhusu hazina itunzwe vipi unazingatia vigezo mbalimbali vikiwemo vile vya kudumisha thamani, wepesi wa kubadilisha pamoja na faida inayopatikana kwa kuwekeza hazina hiyo.
Aidha, Mhe. Kijazi amesema kuwa ununuzi na uuzaji wa madini ya dhahabu unahitaji ujuzi maalum ambapo kwa kuzingatia jukumu la msingi la Benki Kuu inaonyesha dhahiri kuwa Benki hiyo haijajijengea uwezo katika eneo la biashara ya madini hayo. (P.T)
ombo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza waombolezaji katika hafla ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam. Pamoja naye ni Rais Mstaafu Mze Benjamin Mkapa, Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Frederick Sumaye Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Mama Salma Kikwete jana Novemba 10, 2016 PICHA NA IKULU
pole1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimfariji Kaka wa marehemu baada ya kutoa heshima zake za mwisho kwa  mwili wa aliyekuwa Waziri wa Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam jana Novemba 10, 2016
pole2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimfariji mjane wa  marehemu baada ya kutoa heshima zake za mwisho kwa  mwili wa aliyekuwa Waziri wa Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam jana Novemba 10, 2016
pole3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimfariji mtoto wa  marehemu, Jimmy Mungai,  baada ya kutoa heshima zake za mwisho kwa  mwili wa aliyekuwa Waziri wa Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam jana Novemba 10, 2016
pole4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimfariji mtoto wa marehemu William Mungai marehemu baada ya kutoa heshima zake za mwisho kwa  mwili wa aliyekuwa Waziri wa Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Novemba 10, 2016
pole5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wanafamilia baada ya kutoa heshima zake za mwisho kwa  mwili wa aliyekuwa Waziri wa Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam jana Novemba 10, 2016
pole6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wanafamilia baada ya kutoa heshima zake za mwisho kwa  mwili wa aliyekuwa Waziri wa Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam jana Novemba 10, 2016
pole7
pole8
pole9
Sehemu ya familia ya aliyekuwa Waziri wa Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai katika hafla ya kuuaga mwili wa marehemy katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam  jana Novemba 10, 2016 (P.T)

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...
Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...
Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...
Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...
Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...
Soma zaidi
mjengwaapp_copy_4d310.jpg

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.
bshyera11_ba222.jpg

SmartadsMaoni ya Wanakijiji

Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *