Monday, 10 October 2016

MPYA:TAARIFA KUTOKA BODI YA MIKOPO HESLB KWA WAOMBAJI MWAKA WA MASOMO 2016/17,KUHUSU TAREHE UTOAJI WA MAJINA

 Image result for HESLB.GO.TZ
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imekamilisha zoezi la kurekebisha fomu za maombi ya mikopo kwa waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017. Zoezi hilo lilianza tarehe 3 na kumalizika tarehe 7 Oktoba 2016.


Kwa sasa Bodi inaendelea na hatua za awali za upangaji wa mikopo ambapo taarifa za wanafunzi watakaopangiwa mikopo zitatolewa kwenye tovuti ya Bodi www.heslb.go.tz siku chache zijazo.
NB: Bodi inawakumbusha waombaji mikopo wote kuwa makini na watu wasio waaminifu wanaoweza kutumia fursa hii kujipatia fedha isivyo halali.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano,
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *