Friday, 14 October 2016

JINSI YA KUHAMA CHUO ULICHOCHAGULIWA KWENDA CHUO KINGINE 2016/2017

 Image result for tcu.go.tz
Habari zenu,
Kumekuwa na sintofahamu kuhusu utaratibu wa kuhama chuo kwa wanafunzi waliochaguliwa vyuo vikuu mwaka wa masomo 2016/2017.


Kazi ya blogger boy ni kukufanya wewe mdau wangu namba moja kukupa mwongozo ili na wewe uwe mjanja wa kumweleza mwenzako ambae hana taarifa hii.

Tofauti na miaka mingine iliyopita mwaka huu utaratibu wa kuhama chuo umebadilika,na hii kuwafanya watu wengi washindwe nini cha kufanya.

JINSI YA KUHAMA CHUO

Endapo unahitaji kuhama chuo ulichochaguliwa kwenda chuo kingine kutokana na sababu zako mbalimbali ikiwemo kuchaguliwa kozi ambayo hujachagua,au kukosa chuo kutokana na competition ktk chuo ulichoomba first round au 2nd round!

Unatakiwa kwenda kwenye chuo husika moja kwa moja unachotaka kuhamia na kuuliza kama kuna nafasi,wakikukubalia ,utapata kwani chuo kitachukua jina lako na kulipeleka moja kwa moja TCU kabla ya tarehe 18 november 2016.Then majina yanatakiwa yapelekwe bodi ya mikopo kabla ya november 30 2016.

Nadhani nimeeleweka ,sasa unaweza kuchukua maamuzi sahihi!
Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *