Monday, 5 September 2016

‘Tumieni mafunzo ya JKT kujiajiri’


MKUU wa Mkoa Kigoma, Brigedia Jenerali mstaafu, Emmanuel Maganga amewataka vijana wanaomaliza mafunzo katika kambi mbalimbali za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) nchini , mafunzo hayo yawe kama nyenzo ya kujiajiri na kuanzisha shughuli mbalimbali za uzalishaji mali.
Maganga alisema hayo kwenye kambi ya JKT Bulombora kikosi cha 821 ambapo vijana waliomaliza kidato cha sita walimaliza mafunzo kwa mujibu ya sheria yajulikanayo kama Operesheni Magufuli.
Katika hotuba iliyotolewa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya Uvinza, Mwanamvua Mrindoko, alisema kuwa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa kambi na risala ya wahitimu hao inadhihirisha wazi kwamba katika muda wao kambini hapo wamepata elimu kubwa.
Aliwataka vijana hao kuwa tayari kufanya kazi mahali popote watakapopangiwa kazi, baada ya mafunzo hayo au baada ya kumaliza masomo yao watakapotoka hapo. Maganga aliwataka vijana hao kujiingiza katika shughuli za ujenzi wa Taifa kutokana na mafunzo mbalimbali waliyopata ikiwemo ukakamavu, uzalendo na mafunzo mengine, badala ya kujiingiza kwenye siasa zenye vurugu ambazo hazitakuwa na tija kwa maisha yao ya baadaye.
Mwakilishi wa Mkuu wa JKT nchini, Philipo Mahende alisema kuwa kutokana na umuhimu wa mafunzo hayo hasa kwa vijana wanaomaliza kidato cha sita na kutarajia kujiunga na vyuo au ajira mbalimbali, serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya uendelevu wa mafunzo hayo kwani faida yake ni kubwa kuliko gharama inayotumika.
Alisema pamoja na kuwajenga kimwili kwa kuwa wakakamavu, kuwajenga kiakili kuwa tayari kufanya kazi mahali popote lakini pia kuwajenga katika misingi ya uzalendo, kujituma na kupenda kufanya kazi ili waweze kutumika mahali na wakati wowote serikali inapohitaji kuwatumia vijana hasa katika kulinda amani ya nchi.
Awali Mkuu wa kambi ya JKT Bulombora, Mohamed Mketto alisema vijana 1,164 walimaliza mafunzo hayo kati ya vijana 1,175 walioanza mafunzo.
Alisema katika muda huo waliweza kutayarisha ekari 200 za mahindi, 60 za michikichi, 30 za mihogo na 10 za mboga na matunda.
Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *