Wednesday, 7 September 2016

Nature amsikitikia KR Muller


 Kiongozi wa kundi la Wanaume Halisi, Juma Nature amehudhunishwa na hali aliyokuwa nayo mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva KR Muller akisema inatokana naa kutokusikiliza ushauri wake.
KR Muller ambaye kwa sasa anajitambulisha kama rais wa Rader Entertaiment iliyo chini ya mwanamuziki TID, alfajiri ya Jumapili alikutwa akiwa hajitambui kwa kuzidiwa na kilevi nje ya baa maarufu maeneo ya Mwembeyanga, Temeke.
 Nature amesema alijitahidi kuizuia hali hiyo, lakini kwa bahati mbaya aliondoka bila kuaga katika kundi na kumtaka amuache kwanza afanye mambo yake kwa sababu ya kumshauri kuepukana na makundi mabaya.
Hapo awali KR Muller alikua kwenye kundi moja na Juma Nature pamoja na Dollo lililoitwa Wachuja Nafaka kabla ya TMK na  baadaye walizalisha kundi la Wanaume Halisi.
“Alfajiri nikiwa nyumbani nilipigiwa simu kwamba ndugu yako tumemkuta huku kalewa, hajitambui kwa kuwa yeye alishaondoka kwenye kundi sisi tulibaki wenyewe kwenye kundi na kina Dolo, tukaona si vibaya tukodi taxi impeleke kwake anakoishi sasa,” alisema Juma Nature.
Nature amesema alipopigiwa simu alfajiri ya Jumapili, ilimrudisha kukumbuka ya nyuma namna alivyomshauri kukaa mbali na matendo yasiyofaa na makundi mabaya.
“Binafsi sijachukulia vizuri yeye ni kioo cha jamii na nilishamshauri huko anakohamia, kwa sababu tangu yupo kwetu alikuwa na matatizo, lakini yamezidi tangu aende huko kwa sababu hivi vitu vinasababishwa na makundi, sasa ukiwa unakaa na makundi ambayo watu wanavyoishi ni tofauti na jamii tayari ni tatizo,” amesema Nature.
Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *