MSAFARA WA MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN WAPATA AJALI MKOANI MTWARA,WANNE WAJERUHIWA | MASWAYETU BLOG
Breaking News
Loading...
Millionaire  Ads

Friday, 9 September 2016

MSAFARA WA MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN WAPATA AJALI MKOANI MTWARA,WANNE WAJERUHIWA


Moja ya Gari ambalo lilikuwa kwenye msafara wa Makamu wa Rais, Mama Samia Sukuhu Hassan,namna lilivyo haribika mara baada ya Kuacha njia na kupinduka.

 Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama Samia Suluhu Hassan ambao ulikuwa unaelekea Wilayani Tandahimba ukitokea Ikulu ndogo ya Rais ,mkoani Mtwara, umepata ajali na kusababisha majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali ya rufaa Ligula.

Ajali imetokea mbele kidogo ya kijiji cha Nanguruwe kilichopo halmashauri ya wilaya ya Mtwara Majeruhi walioumia ni dereva  pamoja na wasaidizi wanne wa Makamu Rais.
Majeruhi wa ajali wakipata msaada wa  huduma ya kwanza mara baada ya gari walilokuwa wanasafiria kuacha njia na kupinduka.

Awali kabla ya gari hilo lililobeba wasaidizi wa Makamu wa Rais kuacha njia na kupinduka, gari liliokuwa limebeba waandishi wa habari wa channel ten, startv na clouds tv liliacha njia na nusura kupinduka.

Barabara ya kutoka Mtwara kuelekea Tandahimba si ya kiwango cha kuridhisha na kuruhusu magari kwenda mwendokasi hali iliyosababisha magari hayo kuacha njia na moja kupinduka kabisa na kusababisha majeruhi.
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APPLICATION MPYA YA MASWAYETU BLOG

google+

linkedin

About Author
  • Donec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Sed posuere consecteturDonec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Read More

    0 comments:

     

    About Us