MPYA:TAARIFA KWA UMMA KUTOKA NACTE KUHUSU MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA CHETI NA DIPLOMA VYUO VYA AFYA,KILIMO,MIFUGO,UALIMU NK 2016/2017 | MASWAYETU BLOG
Breaking News
Loading...
Millionaire  Ads

Monday, 12 September 2016

MPYA:TAARIFA KWA UMMA KUTOKA NACTE KUHUSU MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA CHETI NA DIPLOMA VYUO VYA AFYA,KILIMO,MIFUGO,UALIMU NK 2016/2017

 


TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA PILI KATIKA KOZI ZA CHETI NA DIPLOMA KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu wote walioomba kudahiliwa katika kozi mbali mbali za cheti na diploma na Umma kwa ujumla kuwa uhakiki wa uteuzi wa awamu ya pili kwa waombaji wa cheti na diploma umekamilika na kwamba uteuzi huu sasa unaonekana kwenye kurasa binafsi (profile) za waombaji. Hii ina maana kuwa waliochaguliwa sasa wanaweza kuona mahali walipochaguliwa kupitia kurasa zao binafsi.

Hata hivyo, Baraza linaomba radhi kwa kuwa uhakiki wa uteuzi kwa baadhi ya vyuo haujakamilika hivyo Baraza litashindwa kuwaonyesha waombaji wa vyuo hivyo uteuzi wao. Vyuo hivyo ni pamoja na vyuo vya kilimo na uvuvi na baadhi ya vyuo vikuu.
Baraza pia linapenda kuwaarifu waombaji waliofanya maombi kwenye vyuo vya Ualimu vya Serikali kuwa uteuzi kwenye vyuo hivyo bado unasubiri mwongozo wa Serikali na hivyo watafahamishwa mara Baraza litakapopata mwongozo kutoka Wizara yenye dhamana ya Elimu juu ya uchaguzi huo.
Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji
NACTE
Tarehe: 10 Septemba, 2016
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APPLICATION MPYA YA MASWAYETU BLOG

google+

linkedin

About Author
  • Donec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Sed posuere consecteturDonec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Read More

    0 comments:

     

    About Us