Tuesday, 13 September 2016

HIZI HAPA HABARI ZA NDANI ZA MAGAZETI YA LEO JUMANNE SEP TAREHE 13/9/2016


1
2
3
4
5
6
7
8
9
10

Magazeti ya Leo Jumanne

Published in Jamii

' Biafra Stadium' Kinondoni.
Hapo wa pili kutoka kulia ni Brown Costa. Jamaa alikuwa mzuri sans uwanjani hadi akacheza ligi ya Zanzibar. Namwona anayefuatia ni Hamis Malumbo, mmoja wa magolikipa bora wa kiwango cha kuchezea ligi kuu. Hakukuwa na maskauti wa kumwona na kumsajili. Nawaona brothers Mwinyihamisi,ni akina Hoppa, Mohammed na Khatib.
Hawa jamaa familia nzima walikuwa na kipaji cha kusakata soka akiwemo Mangapi na mdogo wao mwingine jina limenitoka. Hapo kulikuwa na akina Abdul Mweta tukimwita Abdu Kiwaka, huyu akaja kuichezea Simba Sc. Tulikuwa na Amri Said, tukimuita ' Gotagota' .
Huyu akaja kuwa beki imara wa Simba SC. Tulikuwa na Ladislaus Shawa. Huyu aliwahi kuwashangaza watazamaji kwenye moja ya mechi zetu alipotoka golini na mpira na kuwapiga chenga wachezaji wote wa timu pinzani na hadi akabaki na kipa na kupachika bao.
Ladis, ambaye alikufa kwa ajali ya pikipiki akaja kuichezea Sigara FC kwenye ligi kuu. Naam, tulikuwa na wengi mahiri kiasi mwenyekiti wenu siku nikiingizwa kutokea benchi, basi, hadi nyumbani niwaambie! Tumetoka mbali.
Maggid.(P.T)

Ndugu zangu,
Kuna wimbo huu wa mchakamchaka;
" Kambona , ah, ah!
Kambona, ameolewa!
Wapi?
Uko Ulaya!
Wivu?
Wamkereketa!"
Utotoni nilipata kuwasikia kaka zetu wakiimba wimbo huo wa mchakamchaka. Nikiwa shuleni nimesoma sana habari za siasa za wakati huo. Bado naendelea kusoma na kujifunza. Katika kusoma kwangu nimeona, kuwa suala la ugomvi wa Oscar Kambona na Julius Nyerere alikuwa rahisi vile kama tulivyoambiwa na hata kuimbiwa. Simulizi za Oscar Kambona zinabaki kwa wengi kuwa ni za upande mmoja.
Hakika, si wengi wenye kufahamu nini hasa kiliwatokea marafiki watatu hawa (Pichani) ; Julius Nyerere, Oscar Kambona na Rashid Kawawa. Kizazi hiki cha sasa cha Watanzania kinaweza kunufaika sana na uelewa wa yaliyojiri katika harakati za kisiasa za wakati huo zilizopelekea uhuru wa Tanganyika na baadae Oscar ' Kujivua' gamba kwa kutokubaliana na rafiki yake Julius juu ya Azimio la Arusha. Kuna maswali ya kujiuliza; Je, ugomvi wa Oscar na Julius ulianzia kwenye Azimio au kabla ya hapo?
Je, umma ulipotoshwa juu ya nini kilichotokea? Ikumbukwe, Oscar na Julius walikuwa marafiki wa kushibana kiasi cha Julius kuwa ' Mpambe' wa Oscar kwenye ndoa yake iliyofanyika London. Je, Rashid alichangia kwenye ' kutoswa' au ' kujitosa' kwa Oscar. Kwamba Oscar aliona hakupata kuungwa mkono na Rashid. Je, Oscar alifanya makosa kwa kuondoka nchini badala ya kubaki na kupambana kwa hoja na rafiki yake Julius?
Je, nianze kuwasimulia machache niliyojitahidsi kuyajua, au niwaache kwanza wengine msimulie mnayoyajua, maana, kuna wanaodhani wanajua na kuna wanaojitahidi kujua. Mie niko kwenye kundi hilo la pili!
Maggid,

Zuma arudisha pesa zilizokarabati nyumba yake

Published in Jamii
Pesa zilizotumiwa kukarabati nyumba ya Zuma zilikuwa ni za mlipa kodi
Pesa zilizotumiwa kukarabati nyumba ya Zuma zilikuwa ni za mlipa kodi
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amerudisha pesa zilizotumiwa kukarabati nyumba yake binafasi jinsi ilivyoamriswa na mahakama.
Mwandishi wa BBC mjini Johannesburg anaripoti kuwa msemaji wa wizara ya fedha amethibitisha kuwa pesa hizo zimepokelewa.
Wizara ya fedha nchini Afrika Kusini ilikuwa imependekeza kuwa Rais Zuma alihitajika kurejesha dola 509,000 kwa serikali, pesa zilizotumiwa kukarabati nyumba yake huko Nkandla.
Makao ya binafsi ya Zuma ya Nkandla
Makao ya binafsi ya Zuma ya Nkandla
Mahakama ya juu zaidi nchini humo ilikuwa imetoa uamuzi mapema mwaka huu, kuwa Zuma alipe dola milioni 23 pesa za umma zizotumiwa kwa nyumba yake mwaka 2009.
Sakata ya Nkandla ilitishia wadhifa wake Zuma. Alikwepa hatua ya kumuondoa madarakani na shinikizo za kumtaka ajiuzulu.
Hata hivyo aliomba msamaha kwa njia ya runinga mwezi Aprili akisema kuwa suala hilo limeleta aibu.BBC

MWENGE WA UHURU ULIPOZINDUA KIWANDA BABATI

Published in Jamii
mw1
Mkurugenzi wa kiwanda cha ukamuaji na usafishaji wa mafuta ya alizeti cha Mukta Agro-Proccesing Co Ltd cha mjini Babati Mkoani Manyara, Bakari Mukta akishika mwenge wa uhuru ulipofika kuzindua kiwanda hicho.(P.T)
zav1
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka mchana tayari kumwakilisha Rais Dkt John Pombe Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Sita wa Zambia Mhe. Lungu uwanja wa Mashujaa kesho Septemba 14, 2016
zav2
zav3
tbi1
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group wakipokea tuzo kutoka kwa Ma Meneja wa viwanda vya TBL Group walipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JKN wa jijini Dar es Salaam wakitokea nchini Afrika ya Kusini.
tbi2
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group wakipokea tuzo kutoka kwa Ma Meneja wa viwanda vya TBL Group walipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JKN wa jijini Dar es Salaam wakitokea nchini Afrika ya Kusini.
tbi3
Ma Meneja na baadhi ya wafanyakazi  katika picha ya pamoja kwenye uwanja wa ndege wa Dar wa Salaam
-Bia ya Safari yatangazwa kinara kwa ubora barani Afrika
Kampuni ya TBL Group imezidi kung’ara kimataifa  kutokana na viwanda vyake vya kutengeneza bia vilivyopo kwenye mikoa ya Dar es Salaam,Mbeya,Mwanza na Arusha kushinda tuzo za juu za kimataifa za SABMiller kwa uzalishaji bora ambapo pia bia aina ya Safari Lager imetangazwa kuwa ni bia bora (Champion Beer) barani Afrika.
Kampuni ya SABMiller imekuwa na utaratibu wa kushindanisha viwanda vyake vilivyopo kwenye nchi mbalimbali na kutoa vigezo vya kushindania kigezo kikubwa kimojawapo kikiwa ni ubora wa bidhaa zinazozalishwa .
Hafla ya kutangaza viwanda vilivvoshinda na kuvipatia tuzo ijulikanao kama SABMiller Africa Technical Awards ilifanyika jana nchini Afrika na kuhudhuriwa na Maofisa waandamizi wa kampuni hiyo wakiwemo mameneja wa viwanda vya bia kutoka kampuni zake tanzu.
Bia aina ya Safari Lager iliyozalishwa katika viwanda vya TBL vya Dar na Arusha ilitangazwa bia bora barani na kutunukiwa tuzo,kiwanda  cha Dar kikiwa kimeshika nafasi ya kwanza na Arusha nafasi ya pili.
Tuzo nyingine ambazo viwanda vya TBL Group vimeshinda ni tuzo ya uzalishaji wa bia bora ya Castle inayojulikana kama
Mick Steward Castle Lager award ambapo kiwanda cha TBL Dar es Salaam kimeshika nafasi ya kwanza,TBL Mbeya nafasi ya pili na TBL Arusha nafasi ya tatu.
Nyingine ni Tuzo ya Upishi Bora wa bia ya mwaka (Brewery of the Year Award),ambapo kiwanda cha TBL Mbeya kimeshika nafasi ya kwanza na kiwanda cha TBL Mwanza kimenyakua nafasi ya pili.Pia kampuni imeshinda tuzo ya kufuata kanuni bora za Ununuzi na Ugavi (Supply Chain and Planning award).
Mkurugenzi wa Ufundi wa TBL Group,Gavin Van Wijk amevipongeza viwanda vyote kwa kuibuka na ushindi wa tuzo kubwa za SABMiller.
“Ushindani ulikuwa mkubwa ukihusisha viwanda vingine kutoka nchi mbalimbali duniani,inafurahisha kuona viwanda vya Tanzania vinachomoza na kushinda tuzo kama hizi,hii inadhihirisha kuwa TBL imejipanga kwenda sambamba na mkakati wa serikali wa kuifanya Tanzania nchi ya viwanda kwa kuwa mafanikio haya yanaletwa na watanzania wenyewe”.Alisema.
Wijk aliwashukuru wateja wote wa bidhaa za TBL Group kwa kuiunga mkono kampuni na aliahidi kuwa kampuni itaendelea kuzalisha bora wakati huo huo ikishiriki kusaidia miradi mbalimbali ya kuboresha maisha ya wananchi hususani katika sekta za kilimo,mazingira,elimu na afya.
Akiongea kwa niaba ya Mameneja wa viwanda vya TBL Group vilivyoshinda tuzo,Meneja wa kiwanda cha Dar es Salaam,Calvin Martin amesema wamefurahishwa kuona viwanda vya Tanzania vinafanya vizuri na kutambuliwa kimataifa “Tuzo hizi zinatokana na mchango wa kila mfanyakazi wa kampuni,tuzidi kuongeza bidii katika kazi tutazidi kufanya vizuri zaidi na tunashukuru wateja wetu wote kwa kutuunga mkono kwa kutumia bidhaa zetu ,tumejipanga kuhakikisha wanazidi kupata bidhaa zetu kwa ubora mkubwa na kwa urahisi popote walipo”.Alisema Calvin.
Wakati huohuo,Mhandisi wa kitanzania,Richmond Raymond ,ambaye alikuwa ni Meneja wa Kiwanda cha TBL cha Mwanza kwa sasa hivi akiwa amehamishiwa nchini Afrika ya kusini kuwa Meneja wa Kiwanda cha  bia cha Polokwane kilichopo nchini Afrika ya Kusini ametunukiwa tuzo maalumu ya kutoa mchango mkubwa kwa kampuni inaojulikana kama SABMiller Brewery Legend  status katika hafla hiyo.(P.T)

Wafanyakazi wa Benki ya Azania tawi la Moshi ,wakishusha Mbuzi kwa ajili ya kutoa zawadi ya siku kuu ya Idd kwa baadhi ya wateja wake pamoja na makundi yenye mahitaji maalumu.

Meneja wa Azania Bank tawi la Moshi ,Hajira Mmambe akimkabidhi zawadi ya Mbuzi mwakilishi wa Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Jafary Michael , Bw ,Bashir Seleman wa kampuni ya Zuhad kwa ajili ya siku kuu ya Idd.

Meneja wa Azania Bank  tawi la Moshi,Hajira Mmambe akikabidhi zawadi ya Mbuzi kwa msimamizi wa kituo cha kulea watoto waishio kwenye mazingira magumu cha Qadria kilichopo kata ya mji Mpya,Alhaji Taqdir Haji Amir kama sadaka ya siku kuu ya Idd.

Baadhi ya watoto wa kituo cha  kulelea watoto cha Qadria kilichopo kata ya Mji Mpya.

Meneja wa Azania Bank akikabidhi zawadi ya Mbuzi kwa mteja wa Benki hiyo Aman Idd Mushi kwa ajili ya siku kuu ya Idd.

Meneja wa Azania Bank tawi la Moshi,Hajira Mmambe pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo wakikabidhi zawadi ya Mbuzi kwa mwakilishi wa kampuni ya Ibra line ,Bi Mosi Shayo kwa ajili ya siku kuu ya Idd.

Meneja wa Azania Bank tawi la Moshi,Hajira Mmambe akizungumza mara baada ya kukabidhi zaadi ya Mbuzi kwa ajili ya siku kuu ya Idd kwa wateja wake pamoja na makundi yenye mahitaji maalumu.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. (P.T)
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo mhe. Nape Moses Nnauye (wa pili kulia) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano (wa pili kushoto) wakati akiwasili katika Uwanja wa Karume kuhitimisha mashindano ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Star Septemba 11, 2016 kushoto ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Bw. Jamali Malinzi.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wanamichezo, wadau wa michezo na wanahabari kabla ya kushuhudia fainali ya mashindano hayo yiliyohitimisha mashindano hayo kwa Vijana chini ya umri wa miaka 17 Airtel Rising Star katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikagua wachezaji wa timu ya Morogoro Boys kabla ya kuanza kwa fainali kati yao na timu ya Ilala iliyofanyika katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikabidhi kikombe kwa nahodha wa Timu ya wasichana ya Temeke walioibuka washindi wa mashindano ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Star kwa upande wa wasichana katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa hutuba katika swala ya Idd El Haji iliyofanyika Viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam leo asubuhi.

 Swala ikiendelea.

Waziri Mkuu alivyojumuika na waislam wenzake katika swala hiyo.

 Sheikh Abdu Kadri akiongoza swala ya Idd El Haji 

 Sheikh Nurudin Kishki akihutubia baada ya swala hiyo.

 Waumini wa dini ya kiislam wakishiriki swala hiyo.


Waumini wa dini ya kiislam wakiswali.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062) (P.T)

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...
Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...
Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...
Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...
Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...
Soma zaidi
mjengwaapp_copy_4d310.jpg

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.
bshyera11_ba222.jpg

SmartadsMaoni ya Wanakijiji

Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *