Monday, 19 September 2016

Ajali Njombe: Basi la New Force la Dar - Songea lapata ajali, watu kadhaa wahofiwa kupoteza maisha

ajali songea
 Basi la New Force kutoka Dar es salaam kwenda Songea limepata ajali baada ya kupinduka eneo la Kifanya kilomita kadhaa kutoka mkoani Njombe.

Ajali hiyo imetokea Septemba 19,2016 majira ya saa moja na dakika 40 usiku.


Inaelezwa kuwa watu 12 (wanawake 8,wanaume 4) wamepoteza maisha huku 9 wakijeruhiwa.

Abiria wa basi hilo wanasema basi  lilikuwa katika mwendo kasi na kwamba lilinusurika kupinduka mara mbili na mara ya tatu ndipo likapinduka.

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe ACP Prudenciana Protas amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *