Monday, 8 August 2016

Viongozi wa Tume ya Utumishi wa Walimu waripoti Tamisemi


Viongozi wa Tume ya Utumishi wa Walimu waripoti Tamisemi
Viongozi wakuu wa Tume ya Utumishi wa Walimu ambao waliteuliwa hivi karibuni na kuapishwa leo na Rais Dkt John Pombe Magufuli wamekwisharipoti katika Ofisi zao zilizopo mjini Dodoma. Aidha Viongozi hao walipata fursa ya kukutana na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo ofisini kwake mjini Dodoma.
Viongozi hao ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu bwana Oliver Mhaiki na Katibu wa Tume hiyo Bibi Winifrida Rutaindurwa.
Pia viongozi hao walipata fursa ya kutembelea ofisi zao na kuongozwa na aliyekuwa akikaimu nafasi ya Katibu wa Tume Bibi Christina Hape ambaye sasa anakuwa Naibu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu.
Kuapishwa kwa Mwenyekiti na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu kunafungua ukurasa kwa taasisi hiyo kuanza rasmi jukumu la kuwahudumia walimu katika masuala mbalimbali huku muundo wa utumishi wa tume hiyo ukihusisha ngazi za chini na juu.
Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *