Monday, 22 August 2016

PROF NDALICHAKO AVINYOOSHEA KIDOLE VYUO VYA VETA

 

WAZIRI wa Elimu, Sayansi naTeknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, ametoa mwezi mmoja kwa Mamlaka ya VETA kufanya tathmini ya mafunzo wanayotoa katika vyuo vyote nchini ili kuona kama yanaendana na matakwa ya serikali ya kuwa na wataalamu watakaofanya kazi kwenye viwanda.

Aliagiza hivyo alipofanya ziara katika chuo cha VETA kilichopo Kipawa, Dar es Salaam, ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake ambazo amekuwa akizifanya katika vyuo hivyo ili kuona namna vinavyotekeleza majukumu.Alisema katika vyuo ambavyo ametembelea amekuta changamoto za kuwepo kwa mashine zilizoachwa bila ukarabati kiais cha kushika kutu na nyingine nzima kutotumika wakati kukiwa na vyuo vinavyozihitaji.

“Ni vizuri kukawa na usawa wa mahitaji katika vyuo vyote vya VETA kwenye kila mkoa, kulingana na uhitaji na si vyuo vingine kuwa na vifaa na vingine kuvikosa”,alisema.

Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *