Wednesday, 31 August 2016

MTANDAO WA WANAFUNZI (TSNP) MKOA WA KIGOMA WATEMBELEA SHULE MBALIMBALI ZA MJINI KIGOMA

 

Mr. Abdul Nondo, ni mratibu wa mtandao wa wanafunzi TANZANIA (TSNP) mkoa wa kigoma. Kuna program ameianzisha ya kuzungukia Shule mbali mbali TANZANIA, 

Mr. Abdul Nondo

kuhamasisha wanafunzi kidato cha 1 hadi cha nne kutimiza wajibu wao, na kuvaa majukumu Yao, na kujifungia Kwa Muda kutekeleza majukumu Yao, kuwa na nidhamu, kujitambua nini wanapaswa kufanya,kuepuka makundi ambayo hayana utaratibu wa kitaaluma,kupanga ratiba yao ya kujisomea, changamoto wanafunzi wengi hawana utaratibu wa kujisomea, wazazi wao mkoa wa kigoma hawana utaratibu wa kufuatilia maendeleo ya watoto wao.

Wanafunzi wengi wapo huru saana kufanya mambo ambayo si ya msingi Kwa Muda huu wakiwa shuleni, ametembelea Shule ya RUBUGA na kirugu sekondari kigoma, wanafunzi wamekiri hayo na wameahidi kubadilika kuanzia leo hii,, hii Ndio kazi ambayo mtandao wa wanafunzi (TSNP), tunayoifanya. Mtandao tumeunda TSNP CLUBS, ili tuendelee kupata taarifa kutoka Shule hizo. Bado tunaendelea na kazi hiyo, baada ya kigoma ni mikoa mingine.


Pia anapenda kushukuru afisa elimu sekondari manispaa ya kigoma ujiji, ndug, Emmanuel L. Kitemi Kwa ushirikiano wake, pia napenda kumpongeza na kumshukuru meya wa manispaa ya kigoma ujiji,ndug, hussein Ruvagwa, Kwa sapoti yake kubwa na kutambua umuhimu wa elimu mkoa wa kigoma, mimi ni Abdul Nondo mratibu wa mtandao wa wanafunzi TANZANIA (TSNP) mkoa wa kigoma, na mjumbe wa idara ya haki na wajibu wa wanafunzi. No 0762 599672, page sauti ya wanafunzi Tanzania

Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *