Majambazi wavamia nyumba ya Q Chief, waiba vitu vya zaidi ya milioni 2 | MASWAYETU BLOG
Breaking News
Loading...
Millionaire  Ads

Friday, 26 August 2016

Majambazi wavamia nyumba ya Q Chief, waiba vitu vya zaidi ya milioni 2


Q Chief amethibitisha nyumba yake kuvamiwa na majambazi na wamefanikiwa kuiba baadhi ya vitu vilivyomo ndani ikiwemo laptop iliyokuwa na baadhi ya colabo zake.
Akiongea nasi, muimbaji huyo amedai kuwa thamani ya vitu vyake vilivyoibiwa ni kama milioni mbili au tatu.
“Watumishi wa shetani wameamua kufanya kitu cha kihistoria, siku zote wanarukaruka mmoja wawili tunapigiza nao kelele wanaondoka lakini this time wamekuja watu kama sita, saba au nane. Wamekuja na mapanga, wamekuja na mafokolisti yale ya kufungua, wamekuja na gari moja nje sasa sijui walikuwa wanataka kubeba kila kitu?,” ameuliza Q Chief.
“Pale sebuleni mavitu mengine yote wamepita nayo na gym ya nondo ilikuwa tulichukua Mlimani kwa sababu ya exercise,” ameongeza.
“Wamepiga maplazma, wamepiga music system yangu nimetoka nayo South Africa, wamepiga laptop ambayo tayari mimi nilikuwa naangalia nafasi ya kujipanga na connection zangu. Wamepiga piga hivi kama tatu point something au mbili point something wamepiga,” aliongeza.
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APPLICATION MPYA YA MASWAYETU BLOG

google+

linkedin

About Author
  • Donec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Sed posuere consecteturDonec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Read More

    0 comments:

     

    About Us