Wednesday, 24 August 2016

Kingunge awaomba Mwinyi, Mkapa kuzungumza na Rais Magufuli


 
Aliyekuwa kada wa CCM, Kingunge Ngombale Mwiru  amewaomba  marais wastaafu, Rais Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa kuzungumza na Rais John Magufuli ili aitishe kikao kati ya Serikali na Chadema kwa ajili ya kusitisha maandamano yaliyopangwa kufanyika Septemba Mosi.
Kada huyo ambaye alijivua uanachama wa CCM  Oktoba mwaka jana kwa madai kwamba chama hicho kinaendeshwa kwa maslahi binafsi, amesema kuwa mazungumzo hayo yataepusha uvunjifu wa amani nchini.
Kingunge ambaye ameomba kwenye jopo hilo wawepo mawaziri wakuu wastaafu, Edward Lowassa na Fredrick Sumaye na wanapaswa kutambua wajibu wao kwa Watanzania na kwamba hawapaswi kukaa kimya wakati hali kama hiyo inaendelea nchini.
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APPLICATION MPYA YA MASWAYETU BLOG
Share:
Post a Comment

Popular Posts

Pages

Blog Archive

Text Widget

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger