Monday, 22 August 2016

DC Iringa awasweka lupango walinzi wa hospitali
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesera amewasweka rumande walinzi wawili wa kampuni ya ulinzi ya Amazon kwa tuhuma za kuwanyanyasa wananchi wanaouguza wagonjwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.

Hatua hiyo imekuja baada ya wanawake watatu, kumwagiwa maji ya baridi na walinzi hao wakati wakiwa kwenye banda la kusubiria wagonjwa waliolazwa, wakiwataka waondoke kwenye banda hilo.

Akizungumza na Mwananchi, Kasesera alisema saa 3.30 usiku wa kuamkia jana, alipokea wananchi waliomfuata nyumbani kwake wakilalamikia ukatili wanaofanyiwa na walinzi hao licha ya kuwa wanauguza wagonjwa wao kwenye hospitali hiyo.


"Niliamua kwenda moja kwa moja hospitali nikakuta wanawake watatu wanatetemeka na baridi kali baada ya walinzi hawa kuwamwagia maji bila huruma kinyume cha sheria, "alisema.
Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *