Saturday, 16 July 2016

TAARIFA KWA WANAFUNZI WOTE WA SUA AMBAO HAWAJAHAKIKIWA NA BODI YA MIKOPO 2016/2017
SOKOINE UNIVERSITY OF AGRICULTURE
OFISI YA MAKAMU WA MAKAMU MKUU WA CHUO TAALUMA (SUA) 14 JULAI,  2016

UHAKIKI KWA WANAFUNZI WA SUA WANAOPATA UFADHILI TOKA
BODI YA MKOPO KWA WANAFUNZI WOTE:
NAPENDA KUWATAARIFU KUWA UHAKIKI ULIOFANYIKA SUA UMEONESHA KUNA WANUFAIKA 388 TOKA SUA KATIKA MWAKA WA MASOMO 2015/16 AMBAO HAWAJAJITOKEZA KUHAKIKIWA KATIKA CHUO CHETU.
HIVYO WIZARA YA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NA MAFUNZO YA UFUNDI PAMOJA NA BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU ZINAWATAKA WANAFUNZI WOTE AMBAO HAWAKUJITOKEZA KUHAKIKIWA WAJITOKEZE KUHAKIKIWA TAREHE 18 JULAI 2016 BILA KUKOSA. UHAKIKI UTAANZA SAA 2:00 ASUBUHI MPAKA SAA 10:00 JIONI. UHAKIKI HUU UTAFANYIKA UKUMBI WA BARAZA LA CHUO ULIOPO  JENGO LA UTAWALA.
WANAFUNZI WATATAKIWA KUJA NA KITAMBULISHO CHA  CHUO NA KITAMBULISHO KINGINE KINACHOTAMBULIKA KITAIFA NA CHENYE PICHA YAKE. KUTOKUTOKEA KATIKA ZOEZI HILI LA UHAKIKI KUTASABABISHA MWANAFUNZI HUSIKA KUFUTIWA UFADHILI WA MKOPO TOKA SERIKALINI.
Prof. P.R. Gillah
NAIBU MAKAMU WA MKUU WA CHUO (TAALUMA)
Nakala kwa:      Mshauri wa Wanafunzi                   Rais wa Wanafunzi, SUA
                         Wawakilishi wa Madarasa Yote
Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *