Friday, 1 July 2016

MPYA: Serikali imezuia Benki kupandisha viwango vya tozo katika miamala yake

Image result for TANZANIA
Mamlaka ya mapato Tanzania 'TRA' imetoa ufafanuzi kuhusu kodi ya ongezeko la thamani kwenye huduma za kifedha kuwa marekebisho ya sheria ya mwaka 2014 yaliyopitishwa na bunge yanayolenga kutoza kodi la ongezeko la thamani kwa kiwango cha 18% kwenye ada ambazo benki inatoza wateja wake kwenye huduma mbalimbali zitolewazo na benki au taasisi za fedha.

TRA wamesema taasisi za fedha wanapoongeza makato ya miamala ya fedha wanakosea kwa kupandishia wananchi kwa kuwa sheria hiyo inahusu fedha ambayo mwanachi alikuwa anakatwa na taasisi hizo ambayo hapo mwanzoni zilikuwa azilipiwi kodi kwa hiyo hizo ndizo zitakazokatwa 18%.

Mfano kama umetoa fedha ukakatwa 1000 na taasisi ya fedha ilikuwa haikatwi kodi lakini kwa sheria hiyo ada hiyo ndio itakatwa 18% na sio mwananchi kuongezewa makato kama ilivyofanyika kwa baadhi ya taasisi za fedha.
Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *