Saturday, 23 July 2016

Kutoka Dodoma: Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi kumthibitisha Dk. Magufuli kuwa Mwenyekiti


Habari wakuu,
Leo Jumamosi, July 23, 2016 ni mkutano mkuu maalum wa chama cha mapinduzi(CCM) kumthibitisha Rais John Magufuli ili awe mwenyekiti mpya wa chama cha mapinduzi kumpokea kijiti mwenyekiti anayeng'atuka, Rais mstaafu, Dokta Jakaya Kikwete.

Wajumbe wengi wako ukumbini tayari kusubiri mkutano uanze rasmi, tuwe sote pamoja kujuzana yanayojiri kutoka Dodoma.

Rais mstaafu, Jakaya Kikwete na Rais Magufuli pamoja na wake zao wameshaingia ukumbini, wamo pia Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na marais wastaafu wa serikali ya muungano.

Mkutano umeanza kwa kuimba wimbo wa taifa na kinachoendelea kwa sasa ni wimbo wa chama cha mapinduzi kumuaga mwenyekiti anayeng'atuka, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete. 


nitakujuza................
Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *