Thursday, 28 July 2016

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis Aanguka Akiendesha Ibada Kanisani..Tazama Video HapaKiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amepata ajali ya kuanguka ghafla alipokuwa akitembea kuelekea kwenye jukwaa lililoandaliwa kwa ajili ya kuendesha ibada, Czestochowa nchini Poland.
Papa Francis mwenye umri wa miaka 79 alisaidiwa kwa haraka na wasaidizi wake na kufanikiwa kuamka na kuendelea na safari hadi kwenye kiti kilichoandaliwa.

Papa Francis alikosa kukanyaga vyema kidato kimoja na akaanguka katika madhabahu matakatifu zaidi nchini humo, madhabahu ya Jasna Gora.

Papa, mwenye umri wa miaka 79, mzaliwa wa Argentina, alionekana akitembea akiwa anatafakari sana, na hakugundua kulikuwa na kidato kimoja kabla ya kufikia altare, shirika la habari la AP limeripoti.

Mapadre waliokuwa karibu naye walikimbia na kumsaidia kuinuka.

Misa iliendelea kama ilivyopangwa na papa alihubiri kwa muda mrefu mbele ya maelfu ya waumini waliokusanyika Jasna Gora katika jiji la Czestochowa, kusini mwa nchi hiyo.

Ibada hiyo ilikuwa ikirushwa moja kwa moja kupitia vituo mbalimbali vya runinga na kuangaliwa na mamilioni ya watu.

Shirika la habari la AFP linasema aliinuka upesi, na hakuonekana kuumia hata kidogo.

Alipoulizwa iwapo Francis aliumia baada ya kuanguka, msemaji wa Vatican Greg Burke ameambia wanahabari “papa yuko salama”.

Papa amewahi kuteleza na hata kuanguka mara kadha awali, na kila mara huwa anainuka peke yake au kusaidiwa na mmoja wa wasaidizi wake, shirika la AP linasema.

Kwa mujibu wa Daily Mail, Papa Francis anasumbuliwa na ugonjwa unaojulikana kama Sciatica, ugonjwa ambao wakati mwingine hushusha maumivu ya ghafla kwenye miguu kutoka mgongoni.
Angalia Video hapa

Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *