Saturday, 4 June 2016

Tanzania imetolewa na Misri michuano ya AFCON 2017 leo June 4

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

June 4 2016 ilikuwa ni siku ambayo timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars itacheza mchezo wake wa tatu wa Kundi G wa kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika 2017 AFCON, kwa kucheza na timu ya taifa ya Misri The Pharaos uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Huu ni mchezo ambao Taifa Stars alikuwa anahitaji ushindi wa aina yoyote ile.
AW1A1848
Huu ulikuwa ni mchezo wa tatu kwa Taifa Stars, lakini ulikuwa ni mchezo wa marudiano na timu ya taifa ya Misri baada ya mchezo wa kwanza kuchezwa Misri June 14 2015 katika mji wa Alexandria na kumalizika kwa Taifa Stars kufungwa jumla ya magoli 3-0, hivyo huu ulikuwa ni mchezo wa kulipa kisasi kwa Taifa Stars, lakini pia ulikuwa ni mchezo wa kutengeneza mazingira ya kufuzu AFCON 2017.
AW1A1922
Hata hivyo timu ya Taifa ya Tanzania licha ya kuwa nyumbani imekubali kipigo cha goli 2-0, , magoli ya Misri yalifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea anayeichezea klabu ya AS Roma ya Italia Mohamed Salah dakika ya 43 na 58, kwa upande wa Tanzania Mbwana Samatta alikosa penati iliyopatikana baada ya Himid Mao kufanyiwa faulo ndani ya 18.
AW1A1859
Kwa matokeo hayo Taifa Stars wanakuwa wametolewa rasmi katika michuano ya kuwania kufuzu AFCON 2017, lakini imebakiza mchezo mmoja wa kukamilisha ratiba itakayocheza September dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles, Misri imefikisha jumla ya point 10, Taifa Stars point moja na Nigeria ina point 2.
Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *