Nuh Mziwanda: Jike Shupa imetokana na vigodoro | MASWAYETU BLOG
Breaking News
Loading...
Millionaire  Ads

Saturday, 25 June 2016

Nuh Mziwanda: Jike Shupa imetokana na vigodoro


Nuh-mziwanda
WAKATI Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ anaanza safari yake ya muziki miaka kadhaa iliyopita, wengi wetu tulikuwa hatuamini kama ipo siku anaweza kufikia hatua ya kufanya muziki mzuri na kuweza kukubalika.
Wengi waliamini atasikika ndani ya muda mfupi, atapotea kama ambavyo wengi wameibuka na kupotea kabla ya kufikia hatua ya kupata umaarufu.
Hata alipojaribu kutupa karata yake kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji Zuwena Mohammed ‘Shilole’, bado watu walikuwa hawaelewi anafanya nini mjini.
Wengi waliamini hata suala la mapenzi ni kiki tu za mjini. Hata alipokuja kuachwa, wengi waliamini pale ndiyo ulikuwa mwisho wa safari yake.
Lakini waswahili wanasema Mungu hamtupi mja wake, licha ya kuachwa kwa vitimbi na Shilole, kusakamwa mitandaoni kuwa alikuwa akitembea na mtu aliyemzidi umri, hatimaye amefanikiwa kufanya wimbo mkali wa Jike Shupa akimshirikisha fundi Alikiba Saleh ‘King Kiba’ ambao kwa sasa ni habari ya mjini.
Wimbo huo umekubalika. Unachezeka na video yake ni kali.
Je, Nuh anazungumziaje suala la kuonekana amemuimba Shilole? Kwa nini aliamua kuimba wimbo huo? Idea ilitoka wapi? Hapa chini pana mambo mengi zaidi:
Kwanza tuambie jina la wimbo wa Jike Shupa umelitoa wapi?
Hilo neno Jike Shupa amelitoa Alikiba wakati anaandika chorus yake.”
Unataka kutuambia haukuwa wimbo wako hadi jina alitoe Alikiba?
Hapana ni wimbo ambao nilikwishaurekodi na chorus yangu nilikuwa nimeifanya nikawa nataka niuachie, lakini nilipotafakari nikaona sijashirikiana na mtu, mashabiki wangu hawajanizoea kwenye kolabo sasa hivi ngoja nirudi kitofauti.
Nikaona bora nimtafute Alikiba, nikamsikilizisha wimbo, akaniambia mbona Nuh huu wimbo umeshaisha  halafu hapa ulivyoimba wewe mbona wimbo mkali, nikamwambia bro’mimi nahitaji sauti yako. Naomba unisaidie.
Kiba ana jina kubwa, hakukuringia wakati unamuomba kolabo?
“Nashukuru Mungu hakuchomoa. Akaniambia poa tutaenda studio, baada ya muda kama wiki mbili, tukaenda studio tukarekodi wakatoa chorus yangu ambayo mimi nilisharekodi, Ali akanza kuandika chorus yake ambayo ndiyo ikapatikana Jike Shupa ndani ya hiyo chorus.
Sasa hii Jike Shupa ina maana gani? Imetokana na nini?
“Jike Shupa ni kitu ambacho pia kilitukumbusha zamani mimi na Ali, sababu tulikuwa ni family friend. Tunachezacheza wote zamani tukienda kwenye vigodoro, kuna wale wanawake ambao hawajatulia tulikuwa tunawaita majike shupa tukiendaenda kwenye vigodoro, kwa hiyo vitu kama hivyo tukaona poa tulitumie kwa sababu tunalijua na ndiyo tumekua nalo, kwa hiyo kwa kifupi Alikiba ndiye alitoa idea ya Jike Shupa. Namshukuru kwa kufanya kitu kikubwa kwangu.
Watu wanasema umemuimba Shilole baada ya kukutenda huko nyuma, unalizungumziaje hilo?
“Just idea tu, japo watu wengine wanasema nimemuimbia mtu, lakini mimi niliimba kwa ajili ya jamii na mashabiki wangu na watu ambao wametuzunguka sababu kama mapenzi si mimi tu nimeumizwa, wapo wengi tu ambao wameumizwa. Sikujiangalia mimi tu lakini niliangalia na mashabiki wangu.
Kati ya warembo waliowahi kukuumiza penzini ni Shilole, hukuhisi kwamba atajisikia vibaya pindi atakaposikiliza wimbo huu?
Muziki ni filings. Kuimba kile kitu ambacho umekipitia. Haijalishi mapenzi na maisha magumu uliyopitia. Mimi nanukuu marehemu Remmy Ongala, alipoimba Kifo alifiwa na mtu wake wa karibu.
Kwa hiyo hivyo ni vitu ambavyo unaimba kwa fillings. So hata mimi nimeimba kitu ambacho kimenitokea. Siwezi kuimba tu kila siku vitu ambavyo vimewatokea watu wengine. Nafikiri ni jambo zuri kuwapa hisia zangu ambazo naamini hata wao ‘wamezifili’.
Sasa unafikiri Shilole anafurahia kile ulichokifanya katika video kuigiza matendo yote mliyoishi naye?
Kama yeye imemuumiza, I don’t  care. Mimi sijali kwa sababu mimi nimewapa hisia mashabiki wangu.
DONDOO:
Jina kamili: Naftal Mlawa
Umri: 24
Ngoma zake zilizobamba: Otea Nani, Zima Taa, Msondo Ngoma, Bilima, Ganda la Ndizi na Hadithi.
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APPLICATION MPYA YA MASWAYETU BLOG

google+

linkedin

About Author
  • Donec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Sed posuere consecteturDonec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Read More

    0 comments:

     

    About Us