Saturday, 11 June 2016

KISESA DEVELOPMENT AGENCY

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


 Mwanafunzi wa chuo kikKIDEA a Dar es salaamu  (UDSM) ambaye pia ni mkazi Wa mkoa Wa simiyu bw. KONDELA NZUNGU, anawaomba wadau wote ambao ni wapenda maendeleo kuisaidia asasi wanayoianzisha ambayo ni KIDEA (KISESA BEVELOPMENT AGENCY) kwa lengo la kupambana na umasikini ikiwemo utoaji Wa elimu hususani katika sekta muhimu katika jamii kwani kumekuwepo na wimbi kubwa la vijana tegemezi " 

tumeamua kuanzisha asasi hii kwa lengo na kuisadia jamii kiujumla hivyo basi kama malengo yetu yatakugusa tunaomba sana ushirikiano wako na support yako ili tuweze kufanikisha hayo malengo tumejaribu kadri tuwezavyo lakini imetuwia vigumu 
\
kwani ni kazi kubwa inahitajika kufanyika" bw KONDELA pia anaomba pia viongozi kutoka simu kutambua umuhimu Wa asasi hii ili kuisadia serikali katika kutatua changamoto kwani wanasiasa wengi wameshindwa kutambua mchango wa vijana walio na malengo ya kupambana na majanga mbalimabali katika jamii. Yafuatayo ni malengo ya KIDEA;

1. elimu kwa jamii kuhusu kilimo cha kisasa ili kuongeza mapato ya mwaka ya wanajamii ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa chakula na kuisaidia jamii kupata mazao ya biashara ili kujikwamua kiuchumi. 


2.KIDEA tutahakikisha kila mtu katika jamii anashiriki katika suala la kilimo na shughuli nyingine za kibiashara .


3.KIDEA kwa kushirikiana  na mashirika, makampuni na serikali na wapenzi mbalimbali wa maendeleo tutaboresha huduma za elimu ilikuongeza upatikanaji na matumizi ya elimu bora ya awali, msingi na sekondari na kukuza machaguo kwa ajili ya elimu ya ufundi na elimu ya watu wazima kwa kuhakikisha yafuatayo;
  Kuhakikisha shule za msingi na sekondari  zina vyumba vya madarasa vya kutosha,
Madawati ya kutosha,
Vifaa vya kufundishia vya kutosha na
Nyumba za walimu za kutosha


(4)  Kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira ili kupunguza milipuko ya magonjwa na kupinga mabadiliko ya hali ya hewa


   (5)Kutoa elimu kwa jamii kuhusu umhimu wa kuwapeleka shule watoto wenye ulemavu wa aina yoyote.


     (6)Kuielimisha jamii juu ya umhimu wa elimu kwa vijana wa kike na kuzuia mila potofu ya kuwaozesha wakati wakiwa bado wanaendelea na masomo yao


(7).Kuielimisha jamii athari ya mimba za utotoni ( chini ya miaka 18


(8). Kutoa elimu ya kupunguza maambukizo mapya ya virusi vya ukimwi (HIV/AIDS)


(9) Kupambana na imani potofu juu ya watu wenye ulemavu (albino ) na vikongwe ambayo inapekea vifo vya watu wa aina hiyo.


(10). KIDEA kwa kushirikiana  na mashirika, makampuni na serikali na jamii tutasadia kupunguza tatizo la maji katika jimbo la kisesa


(11).KIDEA kwa kushirikiana  na mashirika, makampuni na serikali na wapenzi mbalimbali wa maendeleo tutaboresha huduma za afya


(12) Kutoa misaada mbalimbali kwa wajasiliamali wadogowadogo ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi


(13)Kutoa elimu ya athari ya matumizi ya madawaya  kulevya kwa vijana wanaojihusisha


   (14) Kuhamasisha na kuwashauri serekali kuweka mazingira mazuri naSalama ya wanafunzi ya kujifunzia
Kushirikiana na mashirika 


(15) mengine ambayo yana malengo kama haya
Kuwasaidia watu ambao wameumizwa na wazazi wao kuendelea na masomo na kuwachukulia hatua wazazi wa namna hiyo kwa kushirikiana na serikali.
TUNAOMBA SANA MJITOKEZE KATIKA KUTOA SUPPORT ILI KUFANIKISHA MALENGO TAJWA HAPO JUU;
BY KONDELA NZUNGU m/kiti KIDEA 0768509696
Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *