Wednesday, 8 June 2016

Hii hapa bajeti ya Tanzania kwa mwaka wa fedha 2016/17


INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Habari wakuu,
Leo ni siku muhimu itakayoamua mustakabali wa mambo mengi katika nchi yetu kwa kipindi cha Julai 2016 mpaka Juni 2017 kutokana na kusomwa kwa bajeti itakayoamua utekelezaji wa mambo mengi ya msingi ikiwemo kodi na ugharamiaji wa huduma muhimu. Bajeti hii itaendana na kusomwa kwa bajeti zote zilizo chini ya jumuiya ya Afrika Mashariki. Tuwe sote pamoja kujuzana yanayojiri kutoka Dodoma kuhusu bajeti yetu.

Hotuba ya hali ya uchumi iliyosomwa mapema: HOTUBA YA HALI YA UCHUMI MWAKA 2015
=======

YANAYOJIRI MCHANA
Wabunge wameshaingia bungeni na wageni wengi wanaendelea kuwasili ikiwemo viongozi wa dini, mabalozi, viongozi wastaafu maafisa usalama na wengine wanaowakilisha marika mbalimbali katika jamii.

Wabunge wa upinzani wametoka nje baada ya naibu spika kuingia bungeni

Waziri wa Fedha, Philip Mpango ameingia bungeni na mkoba uliobeba nyaraka za bajeti ya jamhuri ya muungano wa Tanzania. Mpango anamshukuru Rais Magufuli kwa kumteua kuwa waziri wa fedha na anawapongeza wengine waliochaguliwa/kuteuliwa katika nafasi mbalimbali za serikali.

Dk. Mpango amesema bajeti imezingatia maoni ya wadau mbalimbali ikiwemo wenye viwanda pia amewashukuru watanzania waliotii Rai ya Rais Magufuli ya kumuombea na kusema bajeti hio ni ya kwanza ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli.

Dk. Mpango amesema bajeti amesema bajeti ina sehemu kuu mbili

 • Kutatua matatizo yanayowakabili wananchi, kufanya mabadiliko makubwa serikalini hususan kuondoa kazi kwa mazoea
 • Kujenga uchumi wa kiwango cha kati kwa uhalisia na kujenga ajira hasa kwa vijana

Dk. Mpango: Kauli mbiu ya bajeti za Afrika Mashariki ni kuongeza uzalishaji viwandani ili kuongeza ajira. Bajeti ya maendeleo imeongezwa mpaka kufikia asilimia 40 kwa mara ya kwanza Tanzania.

Kwa sasa Waziri Mpango anaongolea mapitio ya bajeti ya 2015/16

#Mpango amesema serikali itawasilisha kwa dharula marekebisho ya sheria ya manunuzi ya umma ili manunuzi yaendane na thamani halisi.

Uzalishaji Viwandani
 • Kufikia azma ya viwanda serikali itatekeleza mikakati mbalimbali ikiwemo kulipa fidia kwa ardhi iliyotengwa kwa ajili ya viwanda, kuboresha kupitia viwanda vidogo(SIDO)
 • Serikali itahakikisha viwanda vilivyopo vinafanya kazi ikiwemo
 • Kuchukua hatua stahiki kwa ajili ya wawekezaji wa viwanda walivyobinafsishiwa na serikali.
 • Kuimarisha utoaji wa mikopo kwenye sekta ya viwanda
 • Kuvutia kampuni za nje kuwekeza nchini kwa kuboresha mazingira ya uwekazaji
Utatuzi wa kero za wananchi
 • Rushwa kwenye utoaji wa huduma: Serikali imetenga shilingi 2.5 kuwezesha uanzishwaji wa mahaka za mafisadi.
 • Kutenga pesa kwa ajili ya TAKUKURU ili kutekeleza majukumu yake.
 • Kudhibiti upotevu wa mapato
Wafanyabiashara wanaokaidi kutumia mashine za EFD wanaweza kuzuiwa kufanya biashara nchini kwa miaka 2. Kuanzia July 1 ni marufuku kwa taasisi zote za serikali kufanya biashara na wafanyabiashara wasiotumia mashine za EFD

#Serikali imedhamiria kuondoa kodi kwenye mazao ya kilimo, benki ya kilimo itapanua huduma zake mikoani.

Uchukuzi: Trilioni 2.49 kwa ajili ya upanuzi reli ya kati, ndege mpya na kununua meli na kufanyia ukarabati za zamani. Kuhakikisha TANESCO inakuwa na uwezo kifedha ili lijiendeshe lenyewe.

Elimu: Serikali imetenga trilioni 4.77 sawa na asilimia 22 ya bajeti yote kwa ajili ya elimu ya msingi bila malipo, mikopo elimu ya juu

Maji: Trilioni 1.02 kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa maji ikiwemo ukarabati wa miundombinu ya maji.

Kuboresha mazingira ya kufanya biashara ikiwemo kodi na tozo zinazolalamikiwa, kuboresha huduma za upatikanaji wa mikopo, usambazaji wa gesi asili, kuondoa urasimu na kupambana na rushwa.
 • Serikali imetenga bilioni 2.4 kuboresha makazi ya wazee na watoto
 • Agizo la Rais kupunguza kodi ya mshahara litaanza kutekelezwa Julai mosi
 • Serikali inavipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa nidhamu, utaratibu wa kodi kwenye maduka ya vyombo vya ulinzi utabadilishwa.
Marekebisho kwenye sheria ya kodi
 • Kuondoa kodi kwenye maharage ya soya kwani yalisahauliwa, kuondoa kodi kwenye mbogamboga zote ili kuwezesha upatikanaji wa lishe bora kwa gharama nafuu.
 • Pendekezo la kuondoa kodi kwenye dawa zinazotibu maji.
 • Bidhaa zinazotengezwa Tanzania Bara na kuuzwa Zanzibar zitatozwa VAT na kinyume chake kwani kifungu cha sasa hakina kifungu cha marejesho ya kodi.
 • Kusamehe kodi ya ongezeko la thamani kwenye bima ya vyombo vya usafiri wa anga kukuza sekta ya Anga na mashirika ya kimataifa kutumia mashirika ya bima ya hapa nchini.
 • Hatua hizi zinatarajiwa kuongeza mapato kwa serikali.
 • Kuondoa msamaha wa kodi kwenye kiinua mgongo cha wabunge kinachotolewa kila baada ya miaka mitano.


Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *