Wednesday, 22 June 2016

Babu Wa Miaka 65 Ambaka Mtoto wa Dada Yake na Kumpa Ujauzito Huko Kilimanjaro
Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamtafuta mzee wa umri wa miaka 65 Dominick Kweka wa kijiji cha Kisereni wilayani Hai kwa tuhuma za kumbaka msichana wa miaka 16 ambaye ni mtoto wa dada yake (Mjomba) na kumpa ujauzito ambao sasa una umri wa miezi sita. 
 
Akizungumza  kwa njia ya simu kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Bw Wilbrod Mutafungwa amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kueleza kuwa juhudi za kumsaka zinaendelea ili afikishwe katika vyombo vya sheria. 
 

Bw Mutafungwa amesema, jeshi la polisi katika mkoa huo halitavumilia kuona vitendo vya ubakaji vikiendelea kutokea kwa watu wa aina hiyo ambao wanakatisha maandalizi ya maisha bora ya wanafunzi wasichana. 
 

Msichana huyo ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Nkuu amesema, mjomba wake huyo alimbaka nyumbani kwake wakati alimpopelekea sola kwa ajili ya kuichaji ili apate nafasi nzuri ya kujisomea nyakati za usiku na ameiomba serikali aendelee na masomo baada ya kujifungua. 
 

Baba mzazi wa msichana huyo Bw Kilasauko Nyuki ameiomba serikali imchukulie hatua kali za kisheria mzee huyo mwenye makazi katika kijiji hicho na majiji ya Arusha na Dar es Salaam ambaye inadaiwa ametoroka baada ya tukio hilo.
Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *