Friday, 27 May 2016

Wanafunzi Wamkataa Mwalimu Wao Wakimtuhumu Kulawiti Wanafunzi Wa Kiume Huko Katavi

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Katika hali isiyo ya kawaida wanafunzi wa kiume wanaosoma  kidato cha tano katika shule ya Sekondari Usevya Halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele Mkoani Katavi wamemkataa Mwalimu wao (jina tunalo) wakimtuhumu kuwafanyia vitendo vya ulawiti. 


Wakizungumza kwa masikitiko na waandishi wa habari shuleni juzi jioni Mbele ya Afsa Elimu Mkoa wa Katavi Everest Hunji,baadhi ya manafunzi ambao ni mwenyekiti wa serikali ya wanafunzi wa Sekondari ya Usevya Moshi Ramadhani na Katibu Joniour Mgallah,walisema vitendo anavyofanya mwalimu huyo vimewaathiri kisaikolojia na kudhorotesha ufaulu wao kimasomo.
 
 

''Kwa kweli sisi wanafunzi tunakiri mwalimu ambae jina lake tunalo amekuwa akitumia Madaraka yake ya umakamo mkuu wa shule vibaya,Hususani anapokukamata na kosa hapa shuleni badala ya kukupa adhabu ya kulingana na kosa ulilofanya anakuomba kujamiiana naye huku akijua kuwa anayetaka kufanya naye mambo hayo ni mwanaume na utakapokataa anatishia kukufukuza shule'' ,walisema.
 

Hata hivyo Wanafunzi hao waliendelea kufafanua kuwa mwalimu huyo tayari ameshatekeleza vitendo hivyo vya ulawiti kwa baadhi ya wanafunzi na kuongeza kuwa wapo tayari kutoa ushahidi mahakamani kama kutahitajika kufanya hivyo.

Sambamba na hayo,walisema kuwa mwalimu huyo amekuwa akiwatumikisha wanafunzi katika shughuli zake binafsi za uzalishaji kwa kuwapeleka kufanya kazi kwenye mashamba yake.
 
 

Naye Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mpimbwe Erasto Kiwale ambaye aliambatana na Afsa Elimu Mkoa wa Katavi Everest Hunji alisema Kitendo hicho hakikubaliki na tayari hatua sitahiki zimeshachukuliwa za kumpeleka katika vyombo vya kisheria.Hivyo Wanapomuona mwalimu huyo mitaani wasidhani hajachukuliwa hatua.
 
 

Kwa upande wa Afsa Elimu Mkoa wa Katavi Everest Hunji.Aliwaambia Wanafunzi kuwa watulivu na kuziacha mamlaka husika kulishughulikia suala hilo huku akiwaahidi malalamiko yao yatashughulikiwa ipasavyo.
Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *