Wanafunzi 1,500 Vyuo Vikuu Wanolewa | MASWAYETU BLOG
Breaking News
Loading...
Millionaire  Ads

Wednesday, 4 May 2016

Wanafunzi 1,500 Vyuo Vikuu Wanolewa

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel, imedhamini kongamano la ajira kwa vijana wa chuo kikuu, lenye lengo la kuwaweka pamoja waajiri na waajiriwa watarajiwa, kuwapatia fursa zitakazowasaidia katika kuendesha shughuli za kiuchumi.Kongamano hilo linashirikisha wanafunzi zaidi ya 1,500 kutoka vyuo vikuu nchini. Kuanzia mwaka jana ,Airtel imejikita na kushiriki katika kongamano hilo ili kuendeleza dhamira yake ya kuwawezesha vijana wanaohitimu vyuoni kupata ajira.

Akizungumzia mpango huo, Meneja Rasilimaliwatu wa Airtel, Gabriella Kaisi alisema”Tunayofuraha kuwa sehemu ya mpango huu kwa kushirikiana AIESEC Tanzania lengo likiwa ni kuwafikia na kuwaajiri vijana wenye vipaji kutoka katika vyuo vikuu mbalimbali nchini.

Tunaamini kila kijana ana nafasi ya kufikia ndoto zake na ndio mana tunatoa fursa kwa vijana kufanya kazi pamoja nasi. Mwaka jana tuliwawezesha vijana watatu wahitimu kutoka IFM na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupata ajira katika ofisi zetu za Airtel.

Vijana hao ni Abubakar Nassor ambaye anafanya kazi katika kitengo cha masoko, James Kwayu yuko katika kitengo cha Huduma kwa wateja na Gerald Msafiri anafanya kazi katika kitengo cha mauzo.

"Vijana hawa watapata nafasi ya kwenda kufanya kazi nje ya nchi makao makuu ya Airtel nchini Kenya na India kwa miezi miwili kuanzia mwezi wa Mei hadi Julai 2016. Watakaporudi watapangiwa kufanya katika vitengo tofauti ili kupata uzoefu na mwanga zaidi”.

Akizungumzia program hiyo, moja kati ya waliofaidika na mpango katika kitengo cha masoko, Abubakar Nassor alisema “Najisikia furaha kuwa mwanachama wa AIESEC Tanzania kwani kumeniwezesha kupata fursa hii adimu ya ajira, uzoefu katika kazi na nafasi ya kujifunza katika kampuni kubwa ya simu duniani. Nimejipanga vyema kujifunza zaidi katika miezi miwili nitakayokuwa nchini India na Nairobi, naahidi kuitumia fursa hii vyema ili kuweza kuzifikia ndoto zangu”.
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APPLICATION MPYA YA MASWAYETU BLOG

google+

linkedin

About Author
  • Donec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Sed posuere consecteturDonec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Read More

    0 comments:

     

    About Us