Sunday, 22 May 2016

Mwandishi wa Global Makongoro Oging’ Afariki Dunia

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

makongoro

Makongoro Oging’ enzi za uhai wake.
Makongoro (2)
Makongoro Oging’ enzi za uhai wake akimkabidhi msaada wa fedha Kundi Luhende (kushoto) katika Hospitali kuu ya magonjwa ya Saratani ya Ocean Road jijini Dar.
WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, watayarishaji wa magazeti ya Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Championi, wamepata pigo kwa kuondokewa na mfanyakazi mwenzao, aliyekuwa Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Uwazi, Makongoro Oging’ aliyefariki leo jioni baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Marehemu aliugua kwa kipindi kifupi na alikuwa akiendelea kwa matibabu akiwa nyumbani kwake Tabata jijini Dar es Salaam ambapo mauti yamemfika.
Makongoro (1)
Makongoro Oging’ enzi za uhai wake akiwa na wakili Mabere Nyaucho Marando (kushoto).
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Amana kusubiri taratibu za mazishi na msiba upo nyumbani kwake Tabata jijini Dar es Salaam.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.
Mungu ailaze roho ya marehemu Makongoro mahali pema peponi-Amina.
Makongoro (3)
Makongoro Oging’ akiongea na baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Ualimu Chang’ ombe, jijini Dar es Salaam walikuwa katika mgomo.
Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *