Wednesday, 4 May 2016

Mpya: Serikali Kutoa Ajira 71,456

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Serikali inakusudia Kuajili wafanyakazi wapya 71,456, katika mwaka mpya wa fedha 2016/2017 kwa la kujaza nafasi zilizo wazi, huku wilaya ya mbulu ikitengewa nafasi 466.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na utawala bora, Angela Kairuki, aliliambia bunge jana kuwa, maombi ya nafasi za ajira kwa kawaida hufanyika kwa uwazi kupitia bajeti ya seriksli, ambayo huidhinishwa na bunge.
Angela alikuwa akijibu swali la Zacharia Isaya (Mbulu-CCM), Aliyetaka kujua ni lini serikali itajaza nafasi za ajira zilizo wazi katika maeneo mbalimbali nchini kwa ngazi za wizara, mikoa, wilaya na vijiji.
Alisema ajira hizo hufanywa na baada ya waajiri kuwasilisha maombi yao serikalini na kidhinishwa kwa kuzingatia ukomo wa bajeti ya mishahara serikalini.
Waziri alisema kwa halmashauri ya mbulu, katika mwaka wa fedha unaomalizika, ilitengewa kuajiri watendaji wa vijiji (VEO) Kumi na watendaji wa kata (WEO) sita.
Hata hivyo, Waziri alisisitiza kwamba pamoja na nafasi hizo, serikali itajaza nafasi zilizo wazi kila mwaka, kutokana na bajeti itakavyoruhusu na kuzingatia vipaumbele.
Aidha katika kuzingatia kupanda kwa gharama za maisha, Waziri alisema serikali imekuwa ikipandisha kima cha chini cha mshahara kulingana na uwezo wa bajeti, hususani mapato ya ndani.
Kutokana na hatua hiyo, Angela alisema Tanzania ni moja ya nchi za afrika, ambazo kwa sasa hulipa kima cha chini cha mshahara sawa na asilimia 80 ya kiwango cha gharama za maisha (Minimum Living Wage).
Waziri huyo alisema,  serikali itaendelea kuboresha mishahara ya watumishi wake wa umma kulingana na uwezo wa Kiuchumi.
Chanzo: Gazeti la Uhuru
Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *