Mjamzito apigwa chumbani afa! | MASWAYETU BLOG
Breaking News
Loading...
Millionaire  Ads

Tuesday, 24 May 2016

Mjamzito apigwa chumbani afa!

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

YOHANA (5)Marehemu Yohana Albogasti.
Issa Mnally na Richard Bukos, UWAZI
DAR ES SALAAM: Yohana Albogasti, 21, (pichani)mkazi wa Majohe Viwege Kwampemba jijini Dar ameuawa kwa kupigwa risasi chumbani akiwa mtupu, Uwazi limeipata.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo lilijiri usiku wa Mei 13, mwaka huu huko Majohe ambapo marehemu alikuwa ametoka kuoga.
“Mimi nilisikia mlio wa risasi mara moja tu. Nilikuwa na wenzangu, wote tulikaa kimya kila mmoja akihofia kusogelea eneo hilo kwani hatukujua kilichokuwa kikiendelea,” alisema shuhuda mmoja.
Akaendelea: “Kwa kuwa jirani na eneo hilo kuna jumba la kifahari  linalomilikiwa na mfanyakazi wa Tanesco (Shirika la Umeme Tanzania) tulijua majambazi wamevamia kwake.
“Baada ya dakika kadhaa, watu tulianza kwenda eneo la tukio. Ndipo tulipoukuta mwili wa marehemu ukiwa chini hatua chache kutoka nyumba aliyokuwa akiishi.
“Alipigwa risasi chini ya titi la kushoto. Inaonekana alitoka ndani ili kujiokoa lakini alianguka sehemu hiyo akiwa mtupu.”
YOHANA (1)Jirani mwingine aliyedai kushuhudia tukio hilo alisema akiwa eneo hilo alisikia sauti ya mwanamke ikipiga kelele kuomba msaada kisha alimuona mwanaume mmoja akitoweka baada ya mlio wa risasi.
Uwazi pia lilizungumza na mume wa marehemu, Pazi Hamis (23) ambaye alisema:
“Kwa kweli hata mimi nashangaa sana, sijui hawa wauaji walikuwa na kisa gani na mke wangu kwani marehemu hajawahi kuniambia jambo lolote ambalo ningelihusisha na tukio hilo.
YOHANA (2)“Siku ya tukio, saa mbili usiku nikiwa kwenye mihangaiko nilipigiwa simu na jirani na kupewa taarifa. Sikuwa na jinsi, niliwahi eneo la tukio.
“Nilimkuta mke wangu amelala kifudifudi akitoka damu nyingi chini ya ziwa. Polisi nao walifika, wakauchukua mwili hadi Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kuuhifadhi.
YOHANA (3)“Kwangu kifo hiki ni pigo kubwa, kaniachia mtoto Halima ana miaka miwili. Yeye pia alikuwa na ujauzito wa miezi sita.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, SACP Lucas Mkondya alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa mmoja ameshakamatwa, wengine wanasakwa.
 “Mtuhumiwa huyo jina tunalihifadhi kwa ajili ya uchunguzi, mwingine ametoroka.
YOHANA (4)“Tukio lenyewe linaonekana kuwa na utata kwa kuwa marehemu alikuwa akiishi maisha ya hali ya chini, yaani hakuwa na pesa za kuweza kuvamiwa.
“Yawezekana kuna visasi! Hilo ndilo jambo tunaloendelea kulifanyia uchunguzi wakati tukiendelea kumsaka mtuhumiwa aliyetoroka,” alisema Mkondya.
Marehemu amezikwa Jumanne iliyopita kwenye Kijiji cha Kisaki Kata ya Singisa, Matombo mkoani Morogoro.
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APPLICATION MPYA YA MASWAYETU BLOG

google+

linkedin

About Author
  • Donec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Sed posuere consecteturDonec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Read More

    0 comments:

     

    About Us