Monday, 23 May 2016

Kisa Chura… Snura anusurika kichapo

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

snuramushiSTAA wa Muziki wa Bongo Fleva, Snura Mushi ‘Chura’ juzikati akiwa kwenye shoo iliyofanyika Masasi, Mtwara alijikuta katika wakati mgumu baada ya kutaka kupigwa na mashabiki kisa kikiwa eti ni kutokuimba Wimbo wa Chura ambao umefungiwa.
Kwa mujibu wa chanzo, tukio hilo lilijiri mida ya usiku katika ukumbi mmoja maarufu uliopo Masasi ambapo Snura alikuwa akifanya shoo hapo na alipotaka kumaliza, mashabiki walimtaka amalize na Wimbo wa Chura ndipo kizaazaa kilipoanzia na kutaka kumpiga.
Baada ya kunyaka ubuyu huo, Over Ze Weekend lilimnyanyulia simu Snura ambaye simu yake iliita bila kupokelewa lakini alipopigiwa meneja wake, Hemed Kavu ‘HK’ alipokea na kukiri kutokea kwa tukio hilo.
“Siyo tukio moja tu, tulishaenda shoo zaidi ya mbili tunakutana na dhahama hizi. Tatizo lililopo, Snura hawezi kupafomu wimbo ule kwa kuwa ulizuiliwa kutokana na video yake. Ni muda umepita video mpya imetengenezwa na kupelekwa bodi ya filamu kukaguliwa lakini hawajatoa jibu lolote zaidi ya kuzungushwa tu, mara TCRA mara Basata,” alisema HK.
Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *