Monday, 23 May 2016

Jini Kabula Aibu Yake!

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Miriam-Jolwa-Jini-Kabula1Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’.
Aibu yake! Mwigizaji wa kitambo Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amen-aswa akikata ulabu hadi akawa ‘bwii’ huku akiwa amevaa kivazi ambacho kilimuacha nusu utupu hivyo kuibua minong’ono kwa waliomshuhudia.
Tukio hilo la aibu lilijiri wikiendi iliyopita kwenye ‘pub’ moja iliyopo Kijitonyama, Dar ambapo paparazi wetu, akiwa kwenye ‘patroo’ ya matukio alimshuhudia Kabula akiwa ametinga kipensi kifupi kilichoacha sehemu kubwa ya maungo yake nyeti zikiwa wazi.
Paparazi wetu alitonywa kuwa wakati Kabula anatia timu mahali hapo, waliomshuhudia akishuka kwenye Bajaj walishikwa na butwaa baada ya kumuona dada huyo mrefu akiwa nusu utupu huku mwenyewe akiwa hajali.
“Jamani sasa ni aibu…ndiyo tunafahamu kuwa Kabula ni msanii lakini siyo wa kutuvalia vivazi kama hivi huku mtaani. Sasa hapo ana tofauti gani na mtu aliyekaa uchi? Tunamuomba Mungu atuepushe na balaa hili la maadili ya watoto wetu,” alisikika mzee mmoja aliyekuwepo hapo.
Wikienda lilipombana Kabula akiwa tilalila na kumuuliza kulikoni kuvaa nusu utupu, Kabula alidai kwamba aachwe afanye yake.
Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *