Monday, 23 May 2016

DULLY SYKES NA JUMA NATURE KUFANYA SHOW YA KIBABE DAR

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


DullyDully Sykes.
WAKONGWE kwa zaidi ya miaka kumi kunako Muziki wa Bongo Fleva, Dully Sykes, Inspector Haroun, Nature na wengine kibao, Mei 28, mwaka huu wanatarajiwa kulitikisa jukwaa la Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.
nature akiweka mambo sawaJuma Nature
Akichonga na Showbiz, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa mbali na wakali hao, wengine watakaoliteka jukwaa ni Afande Sele, Jafarai, Sister P, Suma G, Abby Skillz na wengineo.
“Hii ni moja ya shoo za kibabe kuwahi kutokea Dar Live pekee. Ambapo niwaambie tu tutakuwa na makundi kibao ya wakongwe ambayo ni Joint Mob, Zig Zag Crew, Solid Ground Family, Mabaga Fresh, Manzese Crew na mengineyo,” alisema Mbizo na kumalizia kuwa kiingilio kitakuwa 7,000 tu getini.
Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *