TAKUKURU Kuwafikisha Mahakamani Kamishna Mkuu wa Zamani wa TRA na Wafanyakazi Wawili wa Stanibic Benki | MASWAYETU BLOG
Breaking News
Loading...
Millionaire  Ads

Saturday, 2 April 2016

TAKUKURU Kuwafikisha Mahakamani Kamishna Mkuu wa Zamani wa TRA na Wafanyakazi Wawili wa Stanibic Benki

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo tarehe 1/4/2016 imewafikisha Mahakamani aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na Mwenyekiti wa ‘Enterprise Growth Market Advisors Ltd’ (EGMA), Bw. Harry Msamire Kitilya; aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Uwekezaji wa Benki ya Stanbic Tanzania, Shose Mori Sinare pamoja na Aliyekuwa Mwanasheria wa Benki ya Stanbic Tanzania, Bw. Sioi Graham Solomon.

Washtakiwa wote wanashtakiwa kwa makosa ya:- Kula njama na kujipatia kwa udanganyifu kinyume na kifungu Na. 384 cha  Kanuni ya Adhabu (Cap 16 R.E. 2002) ; Kughushi kinyume na kifungu Na. 333,335 (a) na 337 cha Kanuni ya Adhabu (Cap 16 R.E 2002) ; Utakatishaji wa fedha haramu kinyume na kifungu Na. 12 (a) 13 (a) cha Sheria ya ya Utakatishaji fedha Na. 12 ya Mwaka 2006 ‘Anti- Money Laundering Act’.

Mashtaka hayo yalisomwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Mhe. Hakimu Emirius Mchauro. Kwa upande wa Jamhuri kesi hii inasimamiwa na Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Serikali Herman Tibabyekomia, Christopher Msigwa na  Mwendesha Mastaka wa TAKUKURU Stanley Luoga. Washtakiwa wanatetewa na Wakili wa Kujitegemea Ringo Tenga, Rosai Mbwambo, Semo na Nyaisa.

Washitakiwa wote watatu wamepelekwa rumande, wamekosa dhamana kwani  Kifungu Na. 148 (5) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) Kinazuia utoaji wa dhamana kwa washtakiwa wa Utakatishaji wa fedha haramu. Kesi hii itatajwa tena tarehe 8/4/2016.

IMETOLEWA NA
OFISI YA AFISA UHUSIANO
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA, MAKAO MAKUU
1 APRIL, 2016.
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APPLICATION MPYA YA MASWAYETU BLOG

google+

linkedin

About Author
  • Donec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Sed posuere consecteturDonec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Read More

    0 comments:

     

    About Us