Thursday, 7 April 2016

TAARIFA KWA UMMA - KUCHELEWA KWA TATHMINI YA VYETI NA ULINGANISHO WA TUZO ZINAZOTOLEWA NA “NCC EDUCATION NA ASSOCIATION OF BUSINESS EXECUTIVES- ABE, UK”

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
 
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
(NACTE)

 

TAARIFA KWA UMMA
KUCHELEWA KWA TATHMINI YA VYETI NA ULINGANISHO WA TUZO ZINAZOTOLEWA NA “NCC EDUCATION NA ASSOCIATION OF BUSINESS EXECUTIVES- ABE, UK”

Baraza la Taifa la Elimu Ufundi (NACTE), linapenda kuujulisha umma kuwa limechelewesha utoaji wa majibu ya maombi ya tathmini ya vyeti na ulinganisho wa tuzo zinazotolewa na NCC Education, UK na Association of Business Executives- ABE, UK kwa kushirikiana na Taasisi binafsi za Elimu ya Ufundi hapa nchini. Hii ni kutokana na kufanya upya uchambuzi wa maombi hayo baada ya kubaini kuwepo kwa dosari katika hatua mbalimbali za utoaji wa mafunzo hayo kama vile sifa za udahili, uendeshaji wa mafunzo, upimaji na vyeti. 

Kulingana na taratibu za Baraza, ni haki ya mwombaji wa huduma hiyo kupewa majibu ndani ya siku 30 baada ya kukamilisha taratibu zote za kutuma maombi. Baraza linatambua kuwa uamuzi wake wa kuchambua upya na tathmini ya maombi yote yaliyotumwa umeleta usumbufu kwa waombaji. Hivyo linaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

Baraza litakamilisha kazi ya kuchambua na kutathmini vyeti na ulinganisho wa tuzo hizo na kutoa majibu kwa waombaji wote kabla ya tarehe 30/04/2016.  
Asanteni kwa ushirikiano wenu.  

IMETOLEWA NA;
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
Tarehe 6/4/2016
Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *