Tuesday, 5 April 2016

Rais Magufuli aombwa kuwa makini na uteuzi wa wakuu wa wilaya

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Watanzania wamemwomba Rais Magufuli kufanya mabadiliko katika Halmashauri za wilaya,manispaa na majiji nchini yakiwemo ya watendaji wake kwa madai kwamba zimejaa ufisadi wa kutisha pengine kuzidi ule wa bandarini.

Dereva taksi mjini Singida,Saad Mhando Mangala,amesema wakati huu Rais Dk.Magufuli akiwa kwenye maandalizi ya kuteua wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmshauri kwa nafasi za ukurugenzi auangalie kwa jicho la kipekee.

Akifafanua,alisema kwenye halmashauri hakuhitaji mtu awe na elimu kubwa ndipo aweze kuwa kiongozi, anatakiwa atambue jinsi rasimali za umma zikiwemo fedha zinavyotumika kinyume na makusudio yake.

“Watendaji katika halmashauri kuanzia mhudumu hadi mkurugenzi wapo vizuri ……wanamiliki mali mbalimbali zilizo nje ya uwezo wa mishahara yao, wakusanya mapato wana vitabu vya stakabadhi mbali mbali,kimoja cha halmashauri na kingine cha kwao na wakubwa wao waliowakabidhi stakabadhi hizo,” alisema.

Akifafanua zaidi, Mangala alisema kwa vile serikali ya awamu ya tano inahitaji watumishi waadilifu,waaminifu na wachapa kazi na upo umuhimu mkubwa safu ya watendaji kuanzia ukurugenzi ikafumuliwa au kufanyiwa mabadiliko makubwa.

“Kwenye halmashauri ambazo ndizo zipo karibu zaidi na wananchi wanatakiwa watendaji kuanzia nafasi ya ukurugenzi na kushuka chini, wawe ni watu watakaoendana na kasi ya utendaji ya Rais Magufuli usio na mzaha na wazembe na wabadhirifu wa mali za umma,” alisema dereva taksi huyo.

Aidha, Mangala alitumia fursa hiyo kumpongeza rais Magufuli kwa uteuzi wake makini wa kuteua wakuu wa mikoa na amemwomba aendeleze utamaduni wake huo wa kuchagua watu wenye elimu stahiki na wawajibikaji katika nafasi ya ukuu wa wilaya.

“Binafsi nisingependa urafiki, ushikaji au sura ya mtu apewe nafasi katia uteuzi wa wakuu wa wilaya. Achanguliwe mkuu wa wilaya mwenye elimu safi na ambaye atamudu kwenda na kasi ya rais wetu Magufuli,” alisema.

Kwa upande wake mkazi wa mjini hapa, Avi Mohammed, alisema wakuu wa wilaya waliopo ambao wameacha kuwatumikia wananchi wakisubiri uteuzi upite wao watumbuliwe na waonyeshwe mlango wa kutokea.

Avi alisema wakuu wa wilaya waliopo madarakani hivi sasa, wanalipwa mishahara kwa kazi ya kuwatumikia wananchi, hivyo kama wameacha kutekeleza majukumu yao ipasavyo watakuwa wanakwenda kinyume na mikataba yao ya kazi.

“Natarajia kuona uteuzi unazingatia watu wenye uwezo wa kukemea na kuwawajibisha watendaji wa chini yao wanao waonea wananchi. Pia wenye kutambua kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu kwa wakati. Wasiteuliwe watu wenye harufu ya rushwa na wavivu,” alisema.

Na Nathaniel Limu, SingidaMkazi wa mji wa Singida, Avi Mohammed, amemshauri Rais Magufuli, asiwateue wakuu wa wilaya ambao kwa sasa hawatekelezi majukumu yao wakisubiri uteuzi.(Picha na Nathaniel Limu)Dereva taksi mjini Singida, Saad Mhando Mangala, amshauri Rais Dk.Magufuli. 
Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *