HABARI NJEMA KWA WALIMU WANAOSUBIRIA AJIRA | MASWAYETU BLOG
Breaking News
Loading...
Millionaire  Ads

Thursday, 14 April 2016

HABARI NJEMA KWA WALIMU WANAOSUBIRIA AJIRA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Selemani Jafo, amewatoa hofu wahitimu wa Kozi ya Ualimu ambao wamekuwa wakisubiri ajira kwa muda mrefu.
Akizungumza leo (JANA) Jijini Dsm Naibu Waziri Jafo amewataka wahitimu hao kuwa na subira kwani ajira hizo zitatangazwa muda wowote kutoka hivi sasa, huku akiwahakikishia kuwa wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu wamejipanga kuhakiki idadi ya walimu wanaohitajika.
Ameongeza kuwa licha ya uhakiki huo pia wizara yake inamalizia takwimu za walimu waliostaafu kazi pamoja na waliohama kutoka shule binafsi ili serikali iweze kujua idadi halisi ya nafasi zinazoitajika.
Jafo ameiambia Mtandao huu kuwa mwaka huu serikali inampango wa kuongeza idadi ya ajira za Walimu hadi kufikia Walimu 40,000 katika ngazi za Shule za Msingi na Sekondari.
Kuhusu ajira hizo Jafo, amefafanua kuwa mikoa ya Kigoma, Mara, Tabora na Rukwa ndio itapewa kipaumbele kwani ndio inaongoza kwa kuwa na idadi ndogo ya Walimu na hii itapunguza kasumba ya wahitimu kozi ya ualimu kupenda kuajiriwa mjini.
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APPLICATION MPYA YA MASWAYETU BLOG

google+

linkedin

About Author
  • Donec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Sed posuere consecteturDonec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Read More

    0 comments:

     

    About Us