Thursday, 24 March 2016

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA MAKAO MAKUU JKT KUHUSU AJIRA KWA VIJANA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
TAARIFA KWA UMMA

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), linakanusha taarifa zilizotolewa kwa Umma kupitia mtandao wa Jamii Forum, tarehe 11 Machi 2016 kuwa, JKT limeanza mchakato wa kuchagua vijana mikoani na wilayani kujitolea kwa nia ya kujiunga na mafunzo ya JKT.
Aidha tangazo hilo linasomeka kuwa mwombaji awe mtanzania mwenye umri wa miaka 18 hadi 23 kwa wenye elimu ya darasa la saba hadi kidato cha sita, miaka 18 hadi 26 kwa wenye stashahada na miaka 18 hadi 35 kwa wenye shahada na kuendelea. Pia asiwe amewahi kuajiriwa na chombo chochote cha Ulinzi na Usalama.

Tangazo hilo kwa umma siyo sahihi na halijatolewa na uongozi wa JKT kama linavyosomeka na kuenezwa kwenye mitandao ya kijamii.
Hadi tarehe 15 Machi 2016 JKT halijaanza mchakato wa kuchukua vijana wa kujiunga na mafunzo ya kujitolea. Muda mwafaka utakapowadia, wananchi watajulishwa rasmi kupitia vyombo vya habari vitakavyoainishwa.
Aidha JKT linazidi kuwakumbusha wananchi kuwa utaratibu wa kuwapata vijana wa kujiunga na mafunzo ya JKT haujabadilika.Maombi yanaanzia wilayani na mikoani kwa kutoa uteuzi wa vijana, kulinagana na nafasi zitakazotolewa kwa kila Mkoa. JKT linaomba wananchi wote kuzingatia utaratibu huo muda utakapowadia.


Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya JKT
Tarehe 15 Machi 2016
Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *