MWANAFUNZI WA CHUO HUKO DODOMA AMUUA MWENZAKE WAKIGOMBANIA CHAJA YA SIMU | MASWAYETU BLOG
Breaking News
Loading...
Millionaire  Ads

Friday, 11 March 2016

MWANAFUNZI WA CHUO HUKO DODOMA AMUUA MWENZAKE WAKIGOMBANIA CHAJA YA SIMU

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Watu wawili wamefariki dunia mkoani Dodoma katika matukio mawili tofauti likiwemo la mwanafunzi wa chuo cha serikali za mitaa Hombolo, Basil Msabila (24) kuuawa kwa kupigwa na chuma kichwani na mwenzake aitwaye Charles Makele (19) kwenye ugomvi wa kugombea chaja ya simu.

Akizungumza na waandishi wa habari, kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa amesema kuwa tukio hilo lilitokea Machi 6 mwaka huu katika chuo cha serikali za mitaa kilichopo Hombolo katika Manispaa ya Dodoma.

Amesema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni ugomvi wa kugombania chaja ya simu ambayo ni mali ya marehemu katika chumba cha bweni ambapo wanaishi wanafunzi wanne.

Katika tukio la pili mtu mmoja mwanaume ambaye hakufahamika jina lake mara moja aliuawa na watu wenye hasira katika eneo la kisasa lililopo katika Manispaa ya Dodoma baada ya kukutwa akivunja dirisha la mtu.

Aidha ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma kutojichukulia sheria mkononi na kutofanya mauaji ya kikatili dhidi ya watu kwa tuhuma nyepesi kwa kisingizio cha watu wenye hasira kali .
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APPLICATION MPYA YA MASWAYETU BLOG

google+

linkedin

About Author
  • Donec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Sed posuere consecteturDonec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Read More

    0 comments:

     

    About Us