Friday, 25 March 2016

Harry Redknapp aiongoza Jordan kushinda goli 8 – 0, Australia nayo yapiga 7 – 0

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Kocha wa zamani wa Tottenham, Harry Redknapp ameiongoza timu ya taifa ya Jordan ambayo ndiyo anayoifundisha kwa sasa, kupata ushindi wa goli 8 – 0 dhidi ya timu ya taifa ya Bangladesh.

Katika mchezo huo wa kutafuta nafasi ya kufuzu kombe la Dunia 2018 Urusi, magoli ya Jordan yalifungwa na Hamza Aldaradreh aliyefunga magoli matatu dk. 23, 29 na 40, Abdallah Deeb dk. 29, Yusef Al Rawashdeh dk. 32, Baha Faisal dk. 62, Atiqur Rahman Meshu dk. 71, Yousef Al Naber dk. 81, Karim Rezaul dk. 83 na Ahmed Samir dk. 90.

Mchezo mwingine ulikuwa kati ya Australia na Tajikistan ambapo Australia imeibuka na ushindi wa goli saba kwa bila.

Baada ya matokeo hayo, Australia inaongoza kundi B ikiwa na alama 18 huku nafasi ya pili ikishikwa na Jordan iliyo na alama 16 na nafasi ya mwisho ikikamatiliwa na Bangladesh iliyo na alama moja. 
Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *