Friday, 26 February 2016

TANZIA:MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU SUA Bsc.IRRIGATION AND WATER RESOURCE ENGINEERING AMEKUTWA KAFARIKI KATIKA PORI

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Ipatapo jana mida ya saa 9 jioni nilipata meseja ikisema  kwamba kuna mwanafunzi kakapotea ni mwaka wa kwanza kozi ya irrigation engineering-sua,wenzako wanaekaa nae room walisema kwamba mwenzao alikuwa ni mgonjwa hivyo siku hiyo aliondoka tangu asubuhi na laiacha simu yake ndani na wakidhani ameenda sehemu ya karibu,hadi kufikia mida ya jioni alikuwa hajarudi.
Leo mida ya mchana huu nimepokea taarifa kutoka kwa mmoja wa viongozi wa hostel zao Mr.hatibu Kilenga ambae amesema kwamba;

"Kwa masikitiko makubwa  napenda kuwajulisha ndugu wana SUA wanafunzi wote ,waafanyakazi na watu wote kwamba leo asubuhimajira ya saa tano asubuhi baada ya heka heka za kumtafuta ndugu yetu YEREMIA MBENDULE,hatimae tumemkuta katika pori la uwanja wa suaakiwa tayari amefariki dunia,tukiwa na polisi tunampeleka marehemu hospitali ya mkoa wa morogoro kwa taratibu nyingine.
Namshukuru Rais wa chuo Mr.Ndunguru,makamu wa Rais na Waziri Mkuu Mr.Salim na wanafunzi wote kwa ujumla kwa jitihada za kumtafuta mpendwa wetu"
Bwana ametwaa jina lake lihidimiwe!AMEN

Marehemu alikuwa ni mwanafunzi wa mwaka wa Kwanza kozi ya Bsc.irrigation and resource engineering na jumatatu alikuwa anajiandaa kuanza mtihani wake wa mwiho wa muhula.

Uongozi wa MASWAYETUBLOG unapenda kutoa pole kwa familia ya marehemu.
Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *