Serikali kutangaza ajira 40,000 za walimu | MASWAYETU BLOG
Breaking News
Loading...
Millionaire  Ads

Tuesday, 16 February 2016

Serikali kutangaza ajira 40,000 za walimu

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
jaffo
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jaffo

Ili kupunguza ukosefu wa walimu katika shule za msingi na sekondari nchini, serikali inatarajia kutoa ajira 40,000 kwa walimu mwaka huu ili kuendana na kasi ya uandikishaji wa wanafunzi na utoaji wa elimu bure.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jaffo, amewaeleza wanahabari kuwa idadi hiyo inalenga kupunguza changamoto ya upungufu wa walimu shuleni na utoaji wa elimu bora zaidi.
Jaffo alisema ajira hizo zitatangazwa mapema mwaka huu na zitaongeza nguvu kwenye shule zenye uhitaji wa walimu hasa mpya na zile zilizoandikisha wanafunzi wengi wa darasa la kwanza na kidato cha kwanza.
Sambamba na hilo, ameahidi kushirikiana na shule za msingi zilizoandikisha wanafunzi wengi zaidi wa darasa la kwanza ili shule hizo zipate miundombinu ya kutosha kuwahifadhi wanafunzi hao.
Amesema kwa kuanza, serikali imejipanga kuongeza majengo katika shule ya msingi Mbagala Majimatitu ambayo imeandikisha wanafunzi wa darasa la kwanza 1,022, idadi ambayo ni sawa na wanafunzi wa shule moja kuanzia darasa la kwanza hadi la saba.
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APPLICATION MPYA YA MASWAYETU BLOG

google+

linkedin

About Author
  • Donec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Sed posuere consecteturDonec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Read More

    0 comments:

     

    About Us