RAIS MPYA WA FIFA NI GIANNI INFANTINO | MASWAYETU BLOG
Breaking News
Loading...
Millionaire  Ads

Saturday, 27 February 2016

RAIS MPYA WA FIFA NI GIANNI INFANTINO

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Gianni Infantino

KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Soka barani Ulaya-Uefa, Gianni Infantino amechaguliwa kuwa Rais mpya wa Shirikisho la Soka duniani-Fifa.

Infantino alishinda awamu ya pilii ya uchaguzi huo uliofanyika Uswisi kwa kura 88 kati ya kura 207 akifuatiwa na Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa wa Bahrain aliyepata 85.

Mwanafalme wa Jordan Ali Bin Hussein alipata kura 27 na mgombea kutoka Ufaransa Jerome Champagne alipata kura saba.

Infantino mwenye umri wa miaka 45 anashika nafasi hiyo kumrithi Sepp Blatter aliyesimamishwa kushiriki shughuli zozote za soka kwa miaka minane adhabu ambayo ilipunguzwa kuwa miaka sita pamoja na Rais wa zamani wa Uefa Michel Platini kwa tuhuma za rushwa.

"Ndugu zangu, siwezi kuelezea hasia zangu kwa wakati huu," Infantino alisema wakati akizungumza baada ya kuchaguliwa. "Tutarejesha hadhi na heshima ya Fifa. Watu watatupongeza, watawapongeza ninyi kwa mabadiliko tutakayofanya.
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APPLICATION MPYA YA MASWAYETU BLOG

google+

linkedin

About Author
  • Donec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Sed posuere consecteturDonec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Read More

    0 comments:

     

    About Us