Tuesday, 23 February 2016

Mapenzi Ndio Basi Tena...Wema Sepetu Afuta Picha zote za Aliyekuwa Mpenzi wake Idris Sultan Kwenye Page yake ya Instagram

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Looks like there is trouble in paradise.. Katika hatua ambayo wengi hawakuitarajia kama ingetokea mapema hivi, Wema Sepetu na Idris Sultan wanaonekana kuuvunja uhusiano wao.
Tetesi za kuwa uhusiano wao upo kwenye mawe zilianza baada ya ujauzito ambao Wema Sepetu alidaiwa kuwa nao kutoka.

Haijulikani ni nani kamkosea mwenzake lakini inaonekana kuwa ni Wema ndiye aliyechukia zaidi kiasi cha kuamua kufuta picha zote za Idris alizowahi kuzipost kwenye akaunti yake ya Instagram.

Wema aliwahi kueleza wazi jinsi ambavyo Idris alikuwa akimpenda Idris na namna alivyomfanya awe mtu mwema.

IDRIS SULTAN: NILIKUWA NAWAPENDA WEMA NA SAMANTHA KWA WAKATI MMOJA, ‘I WAS A VERY BAD GUY

Hata hivyo Idris anaonekana bado moyo wake haujamkatia tamaa Miss Tanzania huyo wa zamani. Jumapili alipost picha akiwa naya na kuandika: Only you know how much i love you, the rest doesn’t matter. #BeingAMan.”

Wengi walikuwa wameanza kuvutiwa na uhusiano wao na waliamini kuwa wawili hao wangekuja kuwa miongoni mwa couple zenye nguvu zaidi. Walikuwa wamepanga pia kuja na reality TV show yao.
Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *