Sunday, 17 January 2016

NAKEMEA KWA UDHALILISHAJI UNAOENDELEA DHIDI YA KABILA LA "WASUKUMA"

Habai zenu,
Nikiwa kama blogger ni mwanahabari kupitia mtandao,nimekuwa nikipokea picha mbalimbali kutoka mitandao ya kijamii mfano watsup na facebook zikiwaandika wasukuma kuwa ndi wanao fanya mambo mabaya na tabia ambazo hazieleweki.

Napenda kuchukua nafasi hii kukemea mara moja tabia hizi mbaya kwani wasukuma pia ni kabila kama yalivyo makabila mengine,nimetokea kuishi nao japokuwa mimi sio msukuma ila ni kati ya watu wastaarabu sana,japokuwa picha hizo inaweza kuwa ni utani,lakini kwa hali inavyoendelea nimeona si mbaya nikitoa mawazo yangu kwamba jambo hili sio zuri hata kidogo,fikiria endapo wewe ndio mtumaji wa picha hizo,kabila lako mfano ni mjita au mhehe ,je,unaweza kutuma picha ikimuonesha mwanamke ambae kwa umri ni sawa na mama ako kwa kumdhalilisha?

Jambo hili sio zuri hata kidogo,naombeni wale wote wenye tabia kama hizi muache mara moja,kwani sio picha nzuri katika jamii,NAKUOMBA MH.MAGUFULI INGILIA KTI SWALA HILI AU WAZIRI MWENYE WIZARA HUSIKA SHUGHULIKIA SWALA HILI,kwani hali inazidi kuwa ni mbaya kila kukicha.

Imeandaliwa na kuandikwa na mimi
INNOCENT THE BLOGGER BOY
(MASWAYETU BLOG TEAM)
Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *