Wednesday, 28 October 2015

TANGAZO LA KUHAMA CHUO KWA WANAFUNZI MLIOCHAGULIWA KUJIUNGA VYUO MBALIMBALI 2015/2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Habari yako,
Endapo wewe ni mmoja ya wanafunzi uliechaguliwa kujiunga na chuo chochote TANZANIA kupitia NACTE tafadhali ,endapo utahitaji kuhama  chuo omba uhamisho MAPEMA.


TANGAZO KWA UMMA
WAOMBAJI WA UHAMISHO KWA PROGRAMU ZA AFYA: STASHAHADA NA ASTASHAHADA
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu wote waliochaguliwa kwenye kozi za afya katika ngazi za Astashahada na Stashahada kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) kwamba kutakuwa na utaratibu wa kuhama kupitia kwenye mfumo (CAS). Tunapenda pia kuwaarifu kwamba wale wote ambao wanataka kuhama kutoka kwenye vyuo walivyopangiwa kwenda vyuo vingine itawapasa kutumia utaratibu ule ule kama walioutumia wakati wa kuomba nafasi kwa gharama  ya Tshs. 30,000/=.
Kwa utaratibu huu tunapenda ifahamike kwamba waombaji watashindanishwa kwa kutegemea nafasi zilizopo na sifa za muombaji.
Utaratibu wa uhamisho utaanza  rasmi Jumatano tarehe 28 Oktoba 2015.

Imetolewa na:
Katibu Mtendaji 
Baraza la Taifa la ElimuyaUfundi (NACTE)
28 Oktoba 2015
Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *