Thursday, 29 October 2015

TAARIFA MUHIMU KWA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM) KUBADILISHWA KWA TAREHE YA KURIPOTI CHUONI

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
slide2
Chuo Kikuu cha Dodoma kinasikitika kuwatangazia Wanafunzi wote kuwa, kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa Chuo tarehe za kufungua Chuo zimebadilishwa.
·        Kwa wanafuzi wapya, Chuo kitafunguliwa tarehe 14 Novemba 2015 badala ya tarehe 31 Oktoba 2015
·     Kwa Wanafunzi wanaondelea, Chuo kitafunguliwa tarehe 21 Novemba 2015 badala ya tarehe 7 Novemba 2015 iliyokuwa imetangazwa awali. 
·        Mitihani ya marudio (Suplimentary Examinations) itafanyika kuanzia tarehe 16 hadi 20 Novemba 2015.
Wanafunzi wote mnatakiwa kukamilisha malipo ya ada na malipo mengine kabla ya kuripoti Chuoni. Wanafunzi watakaoshindwa kukamilisha malipo hayo hawatapokelewa Chuoni.
Tunasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza
Imetolewa na Ofisi ya Mahusiano
29 Oktoba 2015

Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *