TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU WANAJESHI NA KURUTA WALIOKFARIKI KWA AJALI KAMBI YA BUROMBOLA -KIGOMA | MASWAYETU BLOG
Breaking News
Loading...
Millionaire  Ads

Saturday, 3 October 2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU WANAJESHI NA KURUTA WALIOKFARIKI KWA AJALI KAMBI YA BUROMBOLA -KIGOMA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 MKUU WA JESHI LA KUJENGA TAIFA, MEJA JENERALI RAPHAEL MUHUGA ATAONGOZA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MIILI YA MAREHEMU ASKARI WAWILI PAMOJA NA VIJANA WATANO WALIOKUWA WANAPATIWA MAFUNZO YA JKT KAMBI LA BULOMBORA WALIOFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA GARI ILIYOTOKEA MKOANI KIGOMA.
TARATIBU ZA KUAGA MIILI HIYO KWA HESHIMA ZOTE ZA KIJESHI ZINAFANYIKA LEO MCHANA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIJESHI JIJINI DAR ES SALAAM NA BAADAE KUSAFIRISHWA KWA MAZISHI KATIKA MIKOA YA MTWARA, MOROGORO, TANGA, SHINYANGA, KIGOMA NA DAR ES SALAAM.
MAJINA YA ASKARI HAO WA KIKOSI CHA BULOMBORA JKT WALIOFARIKI DUNIA KATIKA AJARI HIYO ILIYOTOKEA TAREHE 01 OKTOBA 2015 MAJIRA YA SAA 10 JIONI NI SAJINI AMIDU ALLY KAMBANGA NA PRIVATE ABEL THADEI MAISHA. WENGINE NI VIJANA WALIOKUWA WANAHUDHIRIA MAFUNZO YA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA KUJITOLEA AMBAO NI SERVICEMAN SAID SADALA SAID NA SERVICEMAN EUGEN STEPHANO BUTATI WALIOKUWA KATIKA MAFUNZO OPERESHENI KIKWETE.
MAKAO MAKUU YA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA KUSHIRIKIA NA MAKAO MAKUU YA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA WAMESHAANDAA NDEGE KUBWA YA KIJESHI ITAKAYOSAFIRISHA MIILI YA MAREHEMU HAO NA KULETWA DAR ES SALAAM.
AIDHA KATIKA AJALI HIYO ASKARI WENGINE 23 WAMEJERUHIWA, KATI YAO WAWILI WATAHAMISHIWA HOSPITALI KUU YA KIJESHI LUGALO KWA MATIBABU ZAIDI.
ASKARI HAO WALIKUWA KWENYE GARI LA JESHI AINA YA IVECO 5717 JW09 AMBAPO WALIPATA AJALI MAENEO YA MLIMA WA PASUA UMBALI WA KILOMITA 11 KUTOKA KIGOMA MJINI, WALIKUWA WANAKWENDA KUBADILISHANA ZAMU YA ULINZI KATIKA MOJA YA KITEULE CHA ULINZI KILICHOPO MKOANI KIGOMA.

IMETOLEWA NA

KURUGENZI YAHABARI NA UHUSIANO,

MAKAO MAKUU YA JESHI LA KUJENGA TAIFA,

LEO TAREHE 03 OKTOBA 2015
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APPLICATION MPYA YA MASWAYETU BLOG

google+

linkedin

About Author
  • Donec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Sed posuere consecteturDonec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Read More

    0 comments:

     

    About Us